Veronica Simba,TimesMajira Online. Ngara
SERIKALI imehimiza kukamilishwa kwa wakati, ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Nyakanazi, ili pamoja na manufaa mengine, kiwaondolee wananchi wa Mkoa wa Kagera adha ya kutokupata umeme wa kutosha.
Kamishna Msaidizi wa Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga ametoa maelekezo hayo juzi kwa mkandarasi anayetekeleza mradi huo, Kampuni ya L&T Construction kutoka India.
Akiwa amefuatana na Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Costa Rubagumya pamoja na Mhandisi Mkuu wa Nishati kutoka wizarani, Salum Inegeja amemtaka mkandarasi kutumia mbinu mbalimbali zitakazomwezesha kukamilisha mradi huo ifikapo Februari 2021 kama ilivyo kwenye mkataba.
Mhandisi Luoga amesema kituo hicho, kinategemewa na miradi mingine ya umeme na kwamba pasipo ujenzi wake kukamilika, miradi hiyo pia haitaweza kuwanufaisha wananchi.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapatoÂ