December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mjasiriamali aliyejiinua kiuchumi kupitia biashara ya keki

Na David John timesmajiraonline

WAJASIRIAMALI kote nchini wanapaswa kuchangamkia fursa za mikopo ya wajasiriamali inayotolewa Serikalini kwa lengo kujikwamua kiuchumi na kupata nafasi ya kuchangia uchumi wa nchi Kwa ujumla .

Mwito huo umetolewa septemba 29 kwenye maonyesho ya sita ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita na Cecylia Miraji mjasiriamali ambaye anajishughulisha na mapishi, vitafunwa keki ambaye pia mshindi wa tuzo ya mwanamke kinara wa mapishi lands ya ziwa .

Cecylia ambaye ni mkazi wa mkoa wa Geita mtaa wa Bomani maeneo ya mgodi wa GGML ,amesema kuwa uwepo wa mikopo hasa taasisi za kifedha zinasaidia wajasiriamali kujikwamua kiuchumi na kuendesha familia zao nakwamaba kupitia Nice Creative Cakes na vitafunwa wanawalika wananchi pia kuchangamkia fursa za kupata keki,Bora ,mapambo, na vitafunwa.

Pia amesema kuwa endapo mtu atakopa na akatumia kwa lengo husika ni rahisi kujeresha mikopo hiyo badala yakutumia tofauti na lengo husika.

Kuhusu biashara ya upishi wa keki ambayo imemuwezesha kupata tuzo amesema kuwa kazi hiyo imemfanya kupiga hatua za kinaendelea ikiwemo kulea na kusomesha watoto huku akitaraji kufanya mambo makubwa kupitia biashara hiyo.

“Hii biashara ya vitafunwa na keki inamuwezesha kujikwamua kiuchumi niwashauri wanawake wenzangu wasibweteke watafute walimu wajifunze upishi wa keki na vutafunwa wataendesha maisha waache uoga wakuthubutu”amesema secylia