Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Mwenyekiti Juma Mizungu aliyasema hayo Kata ya Kisutu Wilayani Ilala wakati wa matembezi ya hisani kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan .
“Nawahimiza vijana wangu kuanzia ngazi ya tawi,Kata na ngazi ya Umoja wa vijana wilaya kutokusubiri vyama vya upinzani kukosoa ndipo mjibu badala yake wayazungumzie maendeleo yaliyopo jamii ifahamu kwa kina miradi inayotekelezwa na Rais Samia ” alisema Mizungu.
Mizungu alisema Miradi ipo kuanzia ngazi ya mitaa yetu.
Kiongozi wa UVCCM katika ngazi hiyo ni lazima uiseme wananchi wa eneo lako wajue serikali inavyotekeleza kwani umoja huo una mchango mkubwa kuhakikisha serikali inatekeleza Ilani ya CCM kwa asilimia 100.
“Katika Wilaya ya Ilala, serikali chini ya Rais Dk. Samia, imetekeleza miradi mingi. Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kivule, vituo vya afya nane vinajengwa, ujenzi wa madarasa zaidi ya 300 , barabara na huduma ya maji,”alieema Mizungu.
Alipongeza UVCCM Kata ya Kisutu kwa kuandaa matembezi hayo maalumu kumpongeza Rais Dk. Samia jambo alililosema litamtia moyo Rais kuendelea kufanya vizuri zaidi.
Katibu wa Mafunzo na Chipukizi wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Ummy, alisema vijana wawe mstari wa mbele kumuunga mkono Rais Dk. Samia kwani wao ndiyo wanufaika wakubwa wa miradi inayotekelezwa kuliko wazee.
“Mikutano ya vyama vya siasa imefunguliwa. hoja za wapinzani sasa zitakuwa ni kuikosoa serikali. UVCCM tusisubiri kujibu hoja hizo bali tuseme kabla hawajasema.”
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kisutu Kumail Rizwani alisema matembezi hayo yalilenga kumpongeza Rais Dk. Samia, kutokana na kasi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuboresha uhusiano wa kidipromasia na kupanua wigo wa demokrasia nchini.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti