Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
MKURUGENZI mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman Amesema katika kusherehekea kumbukizi ya kumuenzi Mwanamke mwasisi wa kwanza na kiongozi wa kwanza wa Jumuia ya umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT )Bibititi Mohamed wao kama Oryx wametoa mitungi ya ges 900 ya kupikia Kwa wanawake mamalishe zaidi 1300 kwenye kata 13 zilizopo Ikwiriri Wilayani rufiji mkoani Pwani.
Akizungumzia katika sherehe hizo Zilizofanyika kwenye viwanja vya ujamaa wilayani humo Disemba 2 mwaka huu na kuandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa mkurugenzi Araman Amesema amefurahi kujumuika nao na kukabidhi mitungi hiyo ya ges Kwa wanawake wa Rufiji.
Akikabidhi mbele ya mgeni rasmi wa sherehe hizo Mery chatanda ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa (UWT) Amaran amesema hatua hiyo inatokana na kuunga mkono juhudi za serikali za kuona watanzania wanatumia nishati safi ya gesi ya kupikia na ili Kuepuka matumizi ya Kuni na mkaa unaoleta uharibifu wa mazingira.
“Nimefurahi kuwa hapa na kusherehekea pamoja katika siku hii azimu ya kukumbuki ya mwasisi na kiongozi wa kwanza wa Umoja wa wanawake Tanzanaia UWT, Bibi titi moahmed.hivyo Mimi na timu yangu tumeleta nishati safinya gas ya kupikia kwa ajili ya wananchi wa ikwiriri na Rufiji.”Amesema
Nakuongeza kuwa ” kupika kwenye gesi ya oryx ni kulinda mazingira hasa kuacha kukata miti na zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake na watoto ambao wanaweza kuvuta moshi mbaya unaotokana na matumizi ya kuni
Amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amejipanga kuhakikisha wanawake,watoto, na wanaume wote nchini Tanzania hadi kufikia 2032 wanapata nishati safi ya kupikia
Katika kuhakikishia lengo linafikiwa kupitia mkutano wa Dubai uliowakutanisha viongozi mbalimbali Duniani kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa wa kujadili mabadiliko tabia nchini ambapo pia Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Mpango wa Nishati safi ya kupikia kwa wanawake barani Afrika.
“Sisi kama Oryx Gas Tanzanaia kushirikiana na serikali na Waziri wetu Mohamed Mchengerwa tutatekeleza maono haya ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan”Amesema
Nakusisitiza kuwa ” Oryx inajuvunia kwa kutoa mitungi zaidi ya 15000 yenye thamani ya zaidi ya Sh.bilioni moja za Tanzania na pia kutoa mitungi ya gesi ya oryx kwa wananchi ni kumaanisha kulinda na kuboresha maisha ya wanawake nakuepuka kwenda kuharibu mistu Kwa kukata miti Kwaajili ya kuni za kupikia.
Pia Amesema kulinda elimu ya watoto ambao wanakwenda shule kusoma hivyo badala ya kwenda kukusanya kuni porini na wao kama Kampuni ya Oryx Gas wanatoa suluhisho la kutumia nishati safi kwa kila mtu.
“Kama Oryx Gas Tanzania tunamshukuru Waziri Mchengerwa kwa kufanikisha mpango huu wa nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa Rufiji hususani mama lishe maarufu kama mama ntilie kwa kuwapatia mitungi ya gesi 900.na tutaendelea kufanya hivyo Kwa maslahi ya taifa.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto