November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mitazamo mitatu inayokwamisha hedhi salama kwenye jamii

Na Aveline Kitomary,TimesMajira Online,Dar es Salaam.

HEDHI  ni hali ya mwanamke  kutoka damu ukeni  baada ya kuta za ndani za mji wa mimba kujiengua, au ni muunganiko wa yai ambalo halikurutubishwa pamoja na damu inayotokana na kumomonyoka kwa tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba (uterus).

Utokwaji damu kwa mwanamke unaonesha ukamilifu wa kuweza kuleta kiumbe kingine duniani hivyo tunasema bila hedhi hakuna kiumbe vipya.

Hali hii kwa kawaida hutokea kila mwezi kwa mwanamke na huratibiwa na mzunguko wa homoni.

Katika jamii za kiafrika hedhi imekuwa ikitafrisiriwa kwa namna tofauti tofauti zisizofaa.

Baadhi ya mila na desturi zimekuwa zikiona suala la hedhi kuwa kama laana au mikosi na sio hilo tu bado mijadala ya hedhi imekuwa ya siri zaidi kama mwiko katika jamii.

Katika maeneo mengi na tamaduni  za Afrika, bado suala la mjadala wa hedhi limekuwa la siri kati ya wanawake pekee wakati mwingine kufanywa kuwa suala la miiko  kutokana  na kutokujadiliwa waziwazi.

Hali hiyo inachangia kuwapo kwa changamoto nyingi miongoni mwa wanawake na  wasichana wadogo, ambazo wakati mwingine zinaweza kuwafanya wakakosa kufikia fursa sawa.

Wengine wanadhani kuwa hedhi ni sumu na inaweza kusababisha uharibifu mfano chakula kuchacha au pombe kuwa chungu.

UELEWA WA JAMII UKOJE?

Utafiti ulifanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na TAMISEMI NA Wadu wa hedhi salama mwaka 2019 ulionesha changamoto nyingi ziko katika ngazi ya jamii kutokana na ulewa mdogo.

Utafiti huo ulibainisha kuwa ni asilimia 28 tu ndio wanauelewa thabiti kuhusu hedhi salama.

Takwimu zinaonesha kuwa maeneo mengi hapa Nchini jamii inakosa uelewa wa umuhimu wa hedhi salama.

Maeneo yaliyofanyiwa utafiti na kuonesha ukosefu wa uelewa wa hedhi salama ni pamoja na Halmashauri za Namtumbo, Muleba, Mbeya, Igunga, Temeke, Karatu, Tandahimba, Rorya, Kusini Unguja na Kaskazini Pemba.

Jamii  katika halmashauri hizo  zilionekana inauelewa mdogo juu ya suala la hedhi salama.

Utafiti wa (NIMR) ulionesha kuwa asilimia 60 ya wasichana walionekana kutomudu gharama za taulo za kike.

Licha ya changamoto hizo utafiti pia ulionesha Nchi imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya ajenda ya afya ya hedhi.

HEDHI NI BARAKA

Katika tamko la Wiziri ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto siku ya maadhimisho ya hedhi Duniani MEI 28 kila mwaka ,Waziri wa Afya  Dk Dorothy Gwajima anasema hedhi wanayopata wanawake sio ugonjwa wala laana bali ni uumbaji wa Mungu katika kumkamilisha mwanamke.

Waziri Gwajima anasema “Ni wakati wa kuchukua hatua ili kuhakikisha vifaa vya kujisitiri/taulo za hedhi zinapatikana kwa urahisi na bei nafuu kwa msichana/mwanamke”.

“Siku ya hedhi duniani inaadhimishwa kila mwaka, licha ya mwaka jana kutofanyika kutokana na changamoto ya Covid 19 lakini jumuiya ya Kimataifa imeendelea kufahamishana, kuelimishana na kukumbushana juu ya jambo hili muhimu kwa njia ya mtandao.

Anabainisha kuwa lengo kuu ni kueleza Dunia na Umma wa Tanzania kuwa hedhi sio ugonjwa wala laana bali ni hali ya kawaida na Baraka ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu inayomtokea msichana mara baada ya kuvunja ungo kama ishara ya mabadiliko kwenye mfumo wa maumbile yake ya uzazi.

Waziri huyo anaongeza kuwa tafiti zinaonesha kila siku wanawake zaidi ya milioni 12 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 wanakuwa kwenye Hedhi duniani.

Aidha, Waziri Gwajima anasisitiza Hedhi Salama akimaanisha kwamba msichana au mwanamke anapokuwa katika siku zake anatakiwa kuzingatia mazingira salama na anapata huduma zote muhimu ikiwemo miundombinu ya vyoo vyenye usiri, maji safi, taulo za kike au vifaa salama vya kujisitiri na utupaji salama wa vifaa/taulo za kike zilizotumika.

“kuna baadhi ya wasichana au wanawake wanakua katika mazingira ya kutokua na hedhi salama ambayo inachangiwa na miundombinu duni ya vyoo, kukosekana kwa maji safi na salama, matumizi ya vifaa vya hedhi visivyo salama na utupaji ovyo wa vifaa vilivyotumika.

Hata hivyo, Waziri Gwajima anawashukuru wadau kupitia mtandao wa hedhi salama kuendelea kuhamasisha upatikanaji wa vifaa vya hedhi salama ndani ya nchi kwa unafuu na ubora unaotakiwa ili kila mhitaji kwa makundi yote aweze kutumia.

USIRI /AIBU NI CHANGAMOTO

Mmoja wapo ya changamoto iliyoaainishwa na watoaji elimu kwa jamii kuhusu hedhi ni usiri wa suala hilo katika jamii.

Mwenyekiti jukwaa la hedhi Tanzania, Salvata Silayo anasema licha kuendelea kuongezeka uelewa lakini bado nguvu inahitaji katika kufanya hedhi kuonekana kuwa kitu cha kawaida.

“Hedhi inaaonekana kitu cha usiri na aibu hutawiki kutaja hadharani Kwa mfano wanawake wakiwa katika hedhi wanakatazwa kugusa  baadhi ya vitu au kutumia.

“Wanaambia wasiende kwenye vyanzo vya maji yatakauka ,wasichume mboga kwasababu majani yatakauka au wasiingie jikoni na mengine

“Kwahiyo sisi tunapambana kuvunja ukimya katika jamii kama zamani binti akivunja ungo hakuna mtu anaweza kujua hata mama hawezi kujua labda shangazi ndo aende kuambiwa ,Kulikuwa na imani kwamba ukimwambia mama wa kwanza anaweza akafariki hizi ni mila tofauti.

Silayo anasema changomoto nyingine ni  akinababa kutotakiwa  kujihusisha na hedhi kwa mabinti zao na pia hata wake zao.

“Matarajio yetu watu waone hedhi ni jambo la kawaida na jambo la  Baraka na pia kumwandaa mtoto wa kike aweze kusoma vizuri

“Ndio maana hata shule tunaweka sehemu ya mtoto wa kike kubadilisha na kujisitiri ,Kwa jamii ambayo ina mtazmo hasi waweze kutambua kuwa hedhi ni jambo la kawaida akinababa wawaangalie binti zao na wake zao wawanunulie taulo za kujisitiri,”anashauri Silayo.

HEDHI NI NINI?

Daktari Bingwa wa Masuala ya Magonjwa ya Kinamama na Uzazi Dk Living colman  anasema hedhi  ni ile damu ambayo mwanamke aliyeko katika umri wa kuzaa miaka 15 hadi 45  anapata kila mwezi .

Anasema kuonekana kwa hedhi  inategemeana kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

“Mtu mwingine anaona siku moja, wengine siku saba hadi nane na walio wengi wanaona kwa siku tatu,Utokaji wake  inategemea pia na mtu kuna mwengine anaweza kuweka pedi moja na wengine pedi tatu hadi nne.

Kuhusu maumivu wakati wa hedhi Dk Colman anasema  inategemea na tatizo la homoni au maabukizi katika mfumo wa uzazi.

 “Mfano hapo tunaweza kuzungumzia maumivu ambayo hayatokani na chochote hata wakipima au yanaweza kutokana na kuwepo kwa kitu  mfano tukipima  uwepo wa tatizo ama maambukizi kama PID, uwepo wa uvimbe kwenye uzazi inaweza kusababisha maumivu.

UMUHIMU WA HEDHI

Dk Colman anasema Umuhimu wa hedhi ni ukamilifu kuwa sasa mwanamke anauwezo wa kupata mtoto inamaana asipopata hedhi ni tatizo ambalo linaweza kuwa katika homoni au mwingine anazaliwa hana kizazi kufunga tunaiita uumbaji wakizazi.

.“Ili hedhi iweze kutokea  mfumo wa homoni unatakiwa uwe umebalance vizuri na huo mfumo wa homoni ni matokeo ya uwiano kati ya kianzilishi  cha homoni kinachoanzia kwenye ubongo hadi kwenye mayai.

“Mayai yanaamrishwa kuzalisha homoni ambayo inaenda kuandaa kuamrisha kuwa kila mwezi inaanda sehemu ambayo mtoto anakuja kukaa pale na ikitoke hakuna mtoto basi ile inatolewa  kama heddhi.

MZAZI YUPI ANAPASWA KUHUSIKA

Dk Colman anabainisha kuwa elimu inahaitajika ni  suala namna ambazo familia zinavyoishi na watoto  wa kike ikiwa ni pamoja nakujenga urafiki.

“Inamaana anapokaribia umri huo anatakiwa aelimishwe aambiwe kuwa kutokana na umri huo anaweza kuona mabadiliko kuwa atakutana na hiki na hiki

“Lakini sasa utakuta haambiwi chochote anaona damu tu anakuwa kwenye mshango haelewi yaani anaona kama vile kitu kipya na ugonjwa kukiwa na elimu kutoka kwa wazazi na waalimu kutoa elimu taratibu kulingana na miaka kama miaka tisa hivi ikitokea inakuwa rahisi kwake kuelewa na kutoa taarifa.

“Wazazi wote wawili  bahati mbaya unakuta watoto wa kike ni marafiki wa baba wakati mwingine anaweza kumwambia baba nimeona kitu hiki kwahiyo ni wazazi wote wawili sio busara kwa mzazi mmoja kuwa karibu na mtoto zaidi.

Mwishoo…