Na Allan Vicent, TimesMajira Online, Tabora
MBIO za Mwenge wa Uhuru zimetembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi yenye thamani ya sh bil 4 katika Majimbo 2 yaliyopo katika halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.
Miradi hiyo ipo katika sekta za elimu, afya, barabara, maji, maendeleo ya jamii na uhifadhi mazingira.
Akizungumza baada ya kuzindua miradi hiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Abdallah Shaib Kaim amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta mabilioni ya fedha katika halmashauri hiyo ili kuchochea kasi ya maendeleo ya wananchi.
Alisema dhamira ya Mheshimiwa kumwaga mabilioni hayo ni kuinua maisha ya wananchi na kuwaondolea kero na adha ambazo zimekuwa kikwazo cha kupata huduma bora.
Shaib alifafanua kuwa miradi iliyotekelezwa na inayoendele kutekelezwa na serikali katika vijiji mbalimbali wilayani humo na Mkoa mzima imelenga kujenga ustawi wa jamii mapema.
Aliitaka jamii kutumia vizuri miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za wananchi walipo kodi ili iwe chachu kubwa ya maendeleo yao.
Akitoa neno la shukrani mbele ya Kiongozi huyo katika uwanja wa Barafu ( eneo la mkesha) Mkuu wa Wilaya hiyo Sauda Mtondoo ameishukuru serikali kwa kuwaletea mabilioni ya fedha kwa ajili ya uboreshaji miundombinu ya shule, ujenzi wa shule mpya na huduma za kijamii.
Alisisitiza kuwa Rais ana mapenzi ya dhati kwa wana Igunga na Jamii kwa Ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilayani humo Mafunga Temanya alipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama kwa dhati katika sekta zote ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.
More Stories
RC Mtambi awataka Maofisa kilimo kutoa elimu ya kilimo mseto
Rais Samia kuelekea nchini Brazil kushiriki mkutano wa G20
Rais Samia atoa maagizo ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo