Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
KATIKA hali ya kushangaza, mikutano ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu imezidi kukosa mvuto kutokana na wafuasi, wanachama na Watanzania kwa ujumla kuendelea na shughuli wakati kiongozi huyo akifanya mkutano wake.
Lissu yupo kwenye ziara zake za Kanda ya Ziwa kukutana na wanachama pamoja na Watanzania kama njia ya kujenga chama chao sanjari na kuzungumzia mwelekeo wa Mkataba wa Bandari dhidi ya Dubai Ports World (DPW).
Katika mkutano uliofanyika leo wilayani Bukombe, mkoani Geita, Lissu alishindwa kabisa kuvutia watu wa kwenda kumsikiliza, jambo linaloonesha mwelekeo mbaya wa chama hicho katika ujenzi wa hoja zenye ushawishi.
Lissu anajitokeza hadharani kuzungumza na Watanzania kuhusu mchakato wa uwekezaji wa Bandari.
Hoja inayowatesa Chadema kwa sasa ni namna ya kuwaaminisha Watanzania kuhusu mchakato wa uwekezaji wa bandari huku wakitumia muda mwingi kukashifu viongozi wa serikali na wastaafu hali inayowapa wakati mgumu kuvutia watu kwenye mikutano yao.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba