Na David John,Timesmajiraonline,Mbeya
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umetekeleza Miradi wa Maghala ya kuhifadhia chakula katika Mikoa Nane ya Tanzania ili kuwasaida wakulima kuhifadhia mazao yao.
Miradi hiyo ni ya teknolojia ya kisasa na inatekelezwa katika Mikoa hiyo ili kusaidia utunzaji wa mazao ya wakulima na kuongeza kuwa mikoa hiyo ni pamoja na ya Nyanda za Juu kusini, ambayo ni Songea, Songwe Makambako, Sumbawanga, Katavi, Shinyanga Manyara na Mkoa wa Dodoma.
Hayo yamebainishwa Mkoani hapa na Mhandisi wa mradi huo, Haruna Kalunga alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari walipotembelea banda la Wakala wa majengo Tanzania TBA Kwenye sherehe za maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane 2023.
Mhandisi Kalunga amesema kuwa mradi wa ghala la kuhifadhia chakula Sumbawanga umeanza kutekelezwa mwezi Januari 2020 na umekamilika mwezi Machi 2023 na umeanza kutumika kwa kuhifadhi mazao ya chakula kwa Wakulima.
“Mradi wa Sumbawanga ni wa teknolojia ya kisasa, na unatunza chakula cha walicholima wakulima Tani 21,000 na lengo kuu la mradi huo kutekelezwa kwa Mikoa 20 lakini kwa sasa tumeanza na Mikoa Nane,”amesema Kalunga.
Aidha Mhandisi Kalunga ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo na kufika katika banda la TBA ili kujua mambo mbalimbali ikiwemo gharama za ujenzi pamoja wa nyumba za makazi na taasisi za serikali kwa gharama nafuu.
More Stories
Maandamano ya kuunga mkono Samia, Mwinyi yatikisa Tabora
Haya hapa matokeo yote kabisa ya Form Four
Kisarawe kukata keki Birthday ya Rais Samia