Na Joyce Kasiki, Timesmajiraonline, Dodoma
MIAKA mitatu ya uongozi wa Rais Samia Sulunu Hassan, imepaisha bajeti imepaisha bajeti Wakala wa Barabara za Mijini na vijijini (TARURA) mkoa wa Dodoma kutoka sh.bilioni 12 .74 aliyoikuta baada ya kuingia madarakani na kuiongeza hadi kufikia sh. bilioni 66.276 sawa na ongezeko la asilimia 412.77.
Hayo yamesemwa jana na Meneja wa TARURA Mkoa wa Dodoma, Mhandisi, Edward Lemelo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia.
“Ndyo maana tunasema ni ongezeko la kihistoria kutokana na pesa tulizokuwa tukipata kabla na baada ya Rais Dkt.Samia kuingia madarakani,” amesema Mhandisi Lemelo
Amesema ongezeko kubwa la bajeti ya TARURA mkoani humo limeiwezesha Mamlaka kuongeza mtandao wa barabara .
Amesema mkoa huo una mtandao wa barabara urefu wa kilomita 7540 .9 ,ambapo barabara za changarawe urefu wa kilomita 1,827, barabara za lami zenye urefu wa kilomita 309.71 na barabara za udongo zenye urefu wa kilomita 5,403.69.
Hata hivyo, amesema kutokana na kuongezeka kwa maeneo mbalimbali na mitaa barabara hizo zitaendelea kuongezeka huku akisema ni lazima wafike katika maeneo yote hivyo mtandao utaongezeka zaidi.
Mhandisi Lemelo amesema kumekuwa na ongezeko la bajeti la kihistoria, ambapo awali kulikuwa na kusuasua kwa maboresho ya barabara kutokana na bajeti mdogo iliyokuwa ikitolewa kwa mkoa huo.
Amesema baada ya kuongezewa bajeti hiyo mtandao wa barabara mkoani humo umeimarika.
“Kwa sasa katika mkoa wetu wa Dodoma asilimia 34.7 za barabara mkoa wa Dodoma zinapitika mwaka mzima,zenye hali mbaya ni asilimia 31 kutoka asilimia 60,”amesema.
Mhandisi Lemelo amesema lengo la mkoa huo ni asilimia 85 ya barabara za mkoa wa Dodoma ziwe zinapitika vizuri ifikapo mwaka wa fedha 2025/2026.
Vile vile amesema kumekuwa na uboreshaji vitendea kazi, ambapo Serikali imesaidia katika eneo hilo kwa kununua magari manane.
“Awali TARURA tulikuwa tunaongoza kwa magari mabaya, lakini kwa kipiindi kifupi tumenunua magri manane.”alisema
Aidha, amesema katika wilaya ya Chamwino wamenunua mitambo ya ujenzi wa barabara ili kuwawezesha kutengeneza wenyewe inapotokea dharura lakini pia wameongezewa watumishi kutoka 69 hadi 84 ambao wamerahisisha usimamizi na utendaji kazi wa taasisi.
Vile vile, mhandisi huyo amesema wametekeleza miradi ya vielelezo ukiwemo ujenzi wa barabara mji wa Serikali Mtumba kwa urefu wa kilomita 52 ambapo katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya Mpwapwa wamejenga barabara za zege.
Pia amesema baadhi ya maeneo ya wilaya za Dodoma yamewekwa taa, hivyo kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao hadi usiku.
Ametumia nafasi hiyo kuishukiru Serikali ya awamu ya sita chini Rais Dkt.Samia na kuahidi kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi katika matengenezo ya miundombinu hasa ya barabara ili ziweze kupitika majira yote ya mwaka.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua