November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Sangweni:Wananchi tumieni nishati safi ya kupikia

Na Penina Malundo,Timesmajira

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni amesema kutokana na uwepo wa ugunduzi wa gesi unaoendelea nchini,wananchi wanapaswa kutumia nishati safi ya kupikia.

Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba,Mhandisi Sangweni amesema tayari Pura imeweka malengo ya kutumia nishati safi ya kupikia kufikia asilimia 80 kwa mwaka 2034.

Amesema kufikia asilimia 80 kwa utumiaji wa nishati safi itasaidia kwa kiasi kikubwa watu kutoka kwenye matumizi ya nishati ambayo yamekuwa yakichafua hali ya hewa kama mikaa na kuni.

” Twendeni tukatumia nishati safinya kupikia ambayo haina madhara yoyote kwa kiasi kikubwa,tuachane na matumizi yq mikaa na kuni imekuwa ni miongoni mwa chanzo cha uchafuzi wa hali ya hewa,’amesema Mhandisi Sangweni.

Aidha amesema wamejipanga kufanya tafiti mbalimbali zakuwezesha jambo hili liwezekane kwa kuzalisha kiasi kikubwa cha gesi ambacho kitaweza kuhudumia majumbani,katika magari na kwenye maeneo mengine.

“Mpaka sasa kuna maeneo ambayo tayari yameshagunduliwa gesi ikiweno Mnazi Bay pamoja na Songosongo iliyopo Mtwara, shirika linaendelea na ugunduzi katika maeneo mengine ambayo yana viashiria vya gesi ambapo imebainika ni asilimia 50 ya eneo la Tanzania,”amesema na kuongeza

“Maeneo yenye viashiria ya mafuta SQM 5,034,000 karibu asilimia zaidi ya 50 za eneo la Tanzania,tushafanya tafiti SQKM 160,200 ,ambapo maeneo tuliyofanyia utafiti mengi yapo Pwani kuanzia Kaskazini kwa maana ya Tanga,Kusini na Mtwara kwani eneo hili limeenda mbali zaidi kuingia baharini zaidi ya km 400,”amesema

Aidha amesema kupitia eneo hilo tayari wamepata kibali kutoka Umoja wa Mataifa (UN)na wamegawa vitalu,kwa kuanza ukanda wa Pwani ambapo watakuwa na vitalu ambavyo watavitangaza.

“Tutatangaza maeneo mbalimbali ambayo watavutia wawekezaji kwa ajili yakuja kushirikiana na taasisi pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kwenye kutafuta na ikiwezekana kinachopatikana wakiwekee mkakati wa kukiendeleza,”amesema.