December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi: Wanawake mkoa wa Mbeya wameweka nadhiri kwa Rais Dkt. Samia

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya

UMOJA wa wanawake mkoa wa Mbeya (UWT)umesema kuwa kutiokana na kazikubwa anayofanya Rais Dkt.Samia Sukuhu Hassan wanawake hao wamesemawameweka nadhiri ya dhati wote kwa kuendelea kumsemea vizuri kwawananchi kwa kazi kubwa za maendeleo anazoendelea kufanya ambazozinawagusa wananchi wa nyanja zote hususani wanawake wataendeleakumuunga mkono katika jitihada zake na serikali.

Wamesema kuwa wanaahidi kueleza kazi kwa watanzania popote walipokazi zinazofanywa na Rais Dktk. Samia Suluhu Hassan chini yaserikali .

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge waVitimaalum mkoa wa Mbeya , Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati wamaandano ya kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwaanayofanya ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleoinayoendelea kufanywa katika maeneo mbali mbali hapa nchini ikiwemomkoa wa Mbeya.

Mhandisi Mahundi amesema kuwa katika kudhikisha hilo katika kipindicha uongozi wake Rais Dkt.Samia ameweza kuimarisha miundo mbinu yashule kwa kuupatia mkoa wa Mbeya zaidi ya trion 12 zilizotokana namiradi ya kupambana na Uvico-19,madarasa, 464 ya shule za sekondariyalijengwa na vituo shikizi 172 zilijengwa.

“Lakini pia Rais Dkt, Samia katika kuhakikisha mkoa wetu wa mbeyaunapata maendeleo ya kutoa pia ametoa zaidi ya Bil.2 kwa ajili yaujenzi wa vyumba vya madarasa 131 kwa iidato cha jkwanza kwa mwakaujao mwaka 2023 , ni ukweli usiopingika kuwa wanawake ndiowanaokwenda hospitali zaidi kuliko wanaume tangu ujauzito mpakakujifungua na kulea watoto na kwamba maisha ya wanawake ni hospitalimuda wote , kwa kutambua umuhimu huo Rais Dkt. Samia ameweza kutoafedha kwa halmashauri za Mbarali, busokelo , Mbeya Dc kila wilayaimepatiwa zaidi ya bil., Kyela .500 za ujenzi wa majengo ya woditatu ya mama na mtoto” amesema Mhandisi Mahundi.

Akielezea zaidi Mhandisi Mahundi amesema Rais Dkt samia ametoazaidi ya Trion 1 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za Chunya na Mbeya Dc, Kyela na Rungwe na kuwa Mkoa wa Mbeya umeendelea kupokea fedhanyingi kutoka serikalini kwa ujenzi wa majengo ya huduma za dharura, Mgeni rasmi katika Maandamano hayo Spika wa Bunge na Mbunge wa MbeyaMjini ,Dkt. Tulia Akson amesema kuwa kitendo cha Mbunge wa vitimaalum mkoa wa mbeya kuwapatia mitaji wanawake ni jambo kubwa sanala kuwainua wanawake kiuchumi mkoa wa mbeya .

Aidha amesema kuwa wanawake wana shukrani kubwa kwa Rais Samia kwakitendo cha kujengewa jingo la mama na mtoto kimeleta faraja kubwasana kwa wanawake.

Mary Mbilo ni Mwenyekiti wa chama Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Mbarali amesema kuwa kazi anayofanya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nikubwa hivyo atahakikisha wilaya hiyo katika uchaguzi mkuu 2025 hawapotezi kata hata moja na kura za Rais Dkt . Samia zitakuwa zakumwagika mimi wananifahamu huwa natembea na kilago mkuu wa mkuu waMkoa sitakuangusha.