November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi: Wanawake jiendelezeni kiuchumi

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

NAIBU Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Mb)Mhandisi, MaryPrisca Mahundi amewataka wanawake wenye malengo ya kujiendeleza kiuchumi kutokuwa wabinafsi katika kupeana ujuzi na maarifa ya mafanikio waliyoyapata na kutembea pamoja bila kuwekeana chuki na husuda kwa mafanikio ya mtu mwingine .

Mhandisi Mahundi amesema hayo Juni 23,2024 jijini mbeya wakati akizungumza na umoja wa wanawake wenye malengo katika mkutano mkuu wa kundi hilo ambalo sasa lina mtaji na dhamana ya zaidi ya Mil.600
walizojiwekea.

Akifungua mkutano huo wenye lengo la kufahamiana na wadau ametoa rai kwa wanawake kuendelea kupendana bila kuwa na choyo ya ujuzi na uwezo walionao katika kuhakikisha kila moja anakuwa kibiashara.

“Hakikisheni mnakuwa na upendo na ushirikiano katika kujiletea maendeleo yenu bila ya kuwa na choyo wala ubinafsi kati yenu “amesema Mhandisi Mahundi.

Akitoa salamu kwa umoja huo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Beno Malisa amewataka wanawake wanawake kuunga mkono katika nafasi za uongozi na kusaidiana kibiashara pasipo kuingia katika mikopo umiza.

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake waliojiwekea malengo (women with Taget)Doris Luvanda pamoja na mhasisi wa kundi hilo Nasra Haonga wakazungumzia malengo yao ikiwa ni pamoja na kusonga mbele zaidi ili waweze kukua kiuchumi.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa akizungumza na wanawake
Baadhi ya wanawake walioshiriki hafla hiyo ambao ni umoja wa wanawake wenye malengo