November 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi azindua Jukwaa la kitaifa la wadau wa kamisheni yapamoja bonde la mto Songwe

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

IMELEEZWA kuwa Mto Songwe unakabiliwa na changamoto za kuhama ambapo husababisha kuwepo kwa mafuriko ,uharibifu wa mazingira hali
inayopelekea kuhama kwa mpaka kati ya nchi mbili za Tanzania na
Malawi .

Kufuatia changamoto hizo imepelekea jamii inayoishi kwenye bonde hilo
kuishi maisha ya mashaka na wasi wasi mkubwa hususani kipindi cha
msimu wa mvua kutokana na mafuriko ambapo wastani wa hekta 15,000
za mazao na zaidi ya watu 52,000 wanaoishi kwenye eneo hil la bonde
huathirika.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa maji (Mb) Mhandishi Maryprisca
Mahundi wakati wa uzinduzi wa jukwaa la wadau wa ufunguzi wa kikao
cha kwanza cha kamisheni ya pamoja ya bonde la mto Songwe kikao
kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano hoteli ya Mdope uliopo
jijini hapa.

Mhandisi Mahundi amesema kuwa usumbufu wa namna hiyo kwa wananchi
wanaoishi nirani na bonde la mto songwe husababisha upotevu wa mali ,makazi , mashamba na maisha ya wakazi wa eneo hilo kutokana
na changamoto hiyo .

Akielezea zaidi Mhandisi Mahundi amesema kuwa serikali za nchi mbili
zimechukua hatua za kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo na
kwamba kamisheni ya Bonde la mto Songwe linatekeleza programu ya
kuendeleza bon de la mto songwe ambapo lengo lake ni kutatua changamoto za kuhama kwa mto na mafuriko ambayo yamekuwa yakipelekea
wananchi kuishi kwa hofu.

‘’Ndugu zangu lengo la jukwaa hili ni kwa ajili ya majadiliano na
kushauriana kuhusu masuala ya kuendeleza bonde hili ambapo
tunakutanisha wadau mbali mbali ili kubadilishana uzoefu ,
kujengeana uwezo na kujadili masuala mbali mbali na kuweka mikakati
ili kufikia matarajio ya kuwa bonde la mto Songwe litakaloshamiri’’amesema Mhandisi Mahundi.

Hata hivyo Naibu waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema
kuwa programu ya kuendeleza bonde la mto Songwe inakwenda kujenga
bwawa litakozalisha umeme kiaso cha Megawati 180 na kwamba umeme huo
mkubwa utagawanyika kati ya nchi za Tanzania na Malawi kupitia kwenye
gridi za Taifa kwa ajili ya ustawi wa viwanda vilivyoko ndani ya
bonde na jamii kwa ujuma.

Aidha mhandisi Mahundi ameagiza sekretarieti kwa kushirikiana na
wadau kuandaa mpango kazi wa utelekezaji kila mwaka na kuwa hiyo
itasaidia kuweza kujipima katika utekelezaji wa shughuli zilizopo
kwenye mpango na kufanya vikao vyake kila mwaka.

Mwakilishi wa mkurugenzi wa Rasilimali za maji Tanzania , Pamela Temu
amesema kuwa ,lengo la kukutana na jukwaa ni kutokana na changamoto
za mipaka hivyo serikali imeona ni jambo kubwa hivyo jkuanzisha
ushirikiano wa pamoja.

Temu amesema kwamba kamisheni hiyo ilianzishwa mwaka 2007 na
kamisheni hiyo ina nchi mbili ambazo ni Tanzania na Malawi na
ushirikiano kati nchi hizo mbili ulianza toka mwaka 1970 shida kubwa
iliyofanya kuanza kushirikiana ni changamoto za mpaka ambao ni
kilometa 200 toka ziwani kuja uwanda wa juu wa bonde.

Mhandisi Elice Englibet ni Mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la ziwa
Nyasa amesema kuwa kazi kubwa ya kamisheni yam to Songwe ni
kuhakikisha wanakusanya na kuchakata taarifa mbali mbali katika
kusaidia nchi mbili za Malawi na Tanzania katika kutoa maamuzi
yatakayowezesha kuweka vizuri bonde la mto Songwe .

Mhandisi Englibet amesema kuwa kitu kingine ni kutekeleza maamuzi ya
nchi mbili kwa manufaa ya nchi zote mbili , kuandaa kamati mbali
mbali ambazo zitasaidia kutoa maamuzi ya bonde la mto songwe.