Na Esther Macha , Timesmajira Online, Mbarali
NAIBU Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Maryprisca Mahundi amekasirishwa na kusuasua kwa mradi wa maji katika eneo la Mkunywa Kata ya Madibira wilaya ya Mbarali unaogharimu zaidi ya shilingi Milioni 800 ambao ulipaswa kukamilika mwezi machi mwaka huu.
Mradi huo ukitelekezwa na kampuni ya Amtec Consulting Company Ltd lakini mpaka sasa umefikia Asilimia 25.
Mhandisi Mahundi akiwa kata ya Madibira leo kuangalia maendeleo ya mradi huo amesema kuwa kwa mradi huo wa Madibira imekuwa kero kubwa awali walishangazwa kwanini tenki hilo hatumiki na kwamba walihaidi kwenye mkutano wa hadhara kuwa lazima tenki hilo litumike na kwamba haiwezekani fedha za serikali zikachezewa tu bila sababu.
Amesema watu wamejenga tenki lakini halina faida lazima tenki hilo litumike na fedha ziwe na thamani na Mh Rais.Samia anatoa fedha ni imani ya kuwa na upendo kwa Wananchi.
“Mh Mkuu wa wilaya nimesikia maneno yaliyosemwa na viongozi wa mbarali hiki kilio sio chenu peke yenu kwani hata sisi wizara ya maji pamoja na Waziri ,Juma Aweso anachukizwa kuona kuwa bado kuna wakandarasi bado wababaishaji na tumekuwa tikiwakaribisha wakandarasi wazawa kwa lengo la kuona uchumi wa Taifa letu fedha ibaki ndani “amesema Mhandisi Mahundi.
Amesema kuwa lengo hasa la kutumia wakandarasi wazawa ni kuweza kuinuana kiuchumi lakini sio kulea wakandarasi wazembe kama huyu na Mimi nimeona hapa kuna shida na mbaya zaidi Kesho Octoba 27 mkataba unakwisha na bado haonyweshi ushirikiano .
Aidha Mhandisi Mahundi amesema kuwa mkandarasi huyo ameambiwa Naibu Waziri anakuja eneo la mradi lakini ameshindwa hata kutuma mwakilishi wake ambaye anaweza kujibu maswali na kusema kwamba katika hilo halivumiliki na kwasababu haya yote natoa maagizo kwa Meneja wa RUWASA mkoa Eng Hansi hilo nakuachia ww kesho mkataba unaisha hatupo tayari kuongeza tena mkataba.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo amesema haiwezekani kampuni mmoja ikasumbua na watu wakachelewa kupata huduma ya maji ambayo ni uhai na Sasa tunaelekea kiangazi tulitarajia wananchi wa madibira wapate maji safi na salama lakini bado tunazungumzia kutengeneza miundo mbinu .
“Sawa mazingira ni magumu lakini unapokuja kuomba kazi wizara ya maji lazima wadau ukaze kiuno na ufanye kazi kwa bidii sio unakuja kuremba kuremba na naungana na nyie Wana Mbarali mkandarasi huyu hatufai tutafuata taratibu na sheria bila kuathiri serikali ya Rais Samia ukiingizia mzigo wa bila sababu za msingi mkandarasi yule tutamwondoa kwa kufuata sheria na taratibu “amesema Mhandisi Mahundi.
Aidha amebainisha kuwa baada ya kukagua chanzo cha maji na banio la mradi huo Mahundi amesikitishwa na mkandarasi kukaidi wito wake na kushindwa kufika eneo la mradi ilhali muda wa utekelezaji wake ukiwa umemalizika na kama serikali hatuko tayari kuona kwamba mradi unaenda kusuasua zaidi.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Mbarali Bahati Ndingo ameomba kuvunjwa mkataba kwa mkandarasi huyo kwani ripoto inasema mradi huo unaisha mwezi wa Octoba 27 ambayo ni leo hili halikubaliki kwa mkandarasi huyu mnavyoona.
“Mradi huu tunatambia kuwa unathamani ya mil.800 ambapo utanufaisha kata nzima ya Madibira na kunywesha watu zaidi ya 18000 kwa hiyo ni mradi muhimu wa kimkakati na kama inavyoelewa wilaya ya Mbarali Ina changamoto kubwa ya maji ambapo hata nyie wizara ya maji mmekiri kuwa ni wilaya ambazo zimekuwa zikiwachemsha kichwa kuona ni namna gani mtasaidia wilaya hii “amesema.
Awali Meneja wa Wakala wa Maji RUWASA Wilaya ya Mbarali Mhandisi Samwel Hechei ametoa taarifa ya mradi mbele ya Naibu Waziri wa Maji amesema kuwa mradi huo ulisainiwa Agosti 22 mwaka 2022 na utekelezaji wake ulianza September 2022 na ulitakiwa kukamilishanamo mwezi Marchi 2023 lakini mpaka Sasa mradi huo haujakamilika kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kusuasua kwa mkandarasi katika kutekeleza ujenzi huo.
Hata hivyo Mhandisi Hechei amesema kwa mujibu wa nyongeza aliyoomba mkandarasi huyo mkataba unatarajiwa kumalizika October 27 mwaka huu (leo).
Aidha Diwani wa Kata ya Madibira Juma Seleman Msiminyungu amesema mkandarasi ana changamoto nyingi zikiwemo za kushindwa kuwalipa hata wafanyakazi wake.
Mkandarasi anayetekeleza mradi huo amekuwa kikwazo na Wizara ya Maji imesema haitawavumilia Wakandarasi wanaochelewesha miradi bila sababu za msingi na haitasita kuvunja mikataba nao.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu