December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi Mahundi achangia Mil.23 umoja wa wanawake wilaya ya Mbeya

Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya

NAIBU Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ameahidi kuchangia Mil 23 kwa ajili ya miradi ya umoja wa wanawake.

Awali Mbunge huyo alichangia Mil.11 lengo likiwa ni kuendelea kusaidia uimarishaji wa miradi ya wanawake iliyopo mkoani Mbeya .

Amesema hayo wakati akizungumza na wanawake wa Wilaya ya Mbeya ikiwa ni mwendelezo wake wa ziara yake ya kuzungumza na wanawake pamoja kuwezesha miradi ya kiuchumi umoja wa wanawake mkoa wa Mbeya.

Aidha katika hatua nyingine Mhandisi Mahundi ametoa simu mbili na kadi 1000 kwa ajili ya usajili wa wanachama pia amewataka Wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali zaidi akiwataka Wanawake kushikamana ili kumvusha Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa amefanya mambo mengi ukiwemo ujenzi wa shule, zahanati na miundombinu.

“Ndugu zangu wanawake mshikamane pamoja ili tuweze kumvusha Rais Samia kwani amefanya mambo makubwa mengi na ya msingi shime shime tumpambanie mwanamke huyu ni shujaa “amesema Mhandisi Mahundi.

Mbali ya ahadi hizo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapatia vitenge kwa ajili ya sare za huku akiahidi kukarabati ofisi ya Katibu.