December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mahundi:Rais Samia anaendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi

Na Esther Macha,TimesmajiraOline,Mbeya

KATIKA kuhakikisha kuwa Wanawake wanakuwa na shughuli za kuwaingiza kipato  Serikali ya awamu ya sita chini Rais,Dkt.Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwakomboa wanawake wenye kipato cha chini kiuchumi.

Naibu waziri wa Maji na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema leo Oktoba 16 mwaka huu wakati akizungumza kwenye Tamasha la Mama Ntilie Festival 2023,  lililofanyika kituo cha mabasi  Kabwe ambalo limeandaliwa na Mbunge huyo jumla ya Mama  lishe 108 walinufaika.

“Serikali inaangalia suala uwezeshaji kiuchumi wanawake,Mimi kama Mbunge nafanya jitihada zangu kwakugusa makundi yote ya wanawake wa mkoa wa Mbeya katika kuona nakuwa  chachu  na hamasa kubwa ili niwaambie msife moyo na  shughuli mnazofanya ni za thamani kubwa sana zinaweza kuwavusha kwenye familia zenu,” amesema Mha.Mahundi.

Aidha Mha.Mahundi, amesema kuwa aliona awaguse Mama lishe kwani wanahudumia watu wengi  na maeneo tofauti wakiwemo mafundi magari,maofisini,kwa kutambua makundi yote haya akadiriki kugusa makundi haya ya mama lishe kwamba wao ni wa thamani kubwa.

Aidha Mha. Mahundi amesema  kuwa wanapomzungumzia kumsapoti, Rais Samia haimanishi kuwa lazima ukae ofisini kuzunguka kwenye kiti  bali popote ulipo unapofanya kazi ya Maendeleo ni  shukrani tosha kuwa unamsaidia Rais kwasababu unampunguzia kazi kwa watu wanaolia njaa.

“Kwa kutambua umuhimu wenu kwenye jamii nikasema nitawapitia mama lishe niwape nguvu kama Mwanamke mwenzenu , Mimi ni mwakilishi wa wanawake wa mkoa wa Mbeya ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wengine huwa hamjui kama tupo tunawawakilisha huwa mnadhani tunawawakilisha CCM wetu ,ukishakuwa kiongozi na uchaguzi ukiisha  tunafanya kazi za Maendeleo bila kuangalia itikadi za vyama “amesema Naibu Waziri huyo.

Suma Mwaikambo ni Mwenyekiti jumuiya ya umoja wa wanawake wilaya ya Mbeya mjini (UWT) amewataka wanawake katika maeneo wanayoishi kuiga mfano wa Mbunge huyo kutokana na kujitoa toka alipoingia kuwa UWT kazi zake zinajieleza na kuwaomba wanawake kutomsahau 2025.

Kwa Upande wake Mwenyekiti UWT mkoa wa Mbeya, Edina Mwaigomole amesema wana viongozi wengi lakini Mha.Mahundi kazi zake zinajieleza zenyewe kwa matendo na kuwa huyo ni mwakilishi wanawake mkoa wa Mbeya kupitia viti maalum sio mwakilishi wa wapiga kura ndiyo sababu anawezesha mama lishe ambao hawafamu kwa sura na kusema wanawake twende tukue pamoja hataki kwenda peke yake kwa kubadilika kiuchumi kwa kutumia rasimali zake kubadilika.

Katika mkutano huo Mhandisi Mahundi ameweza kugawa majiko ya Gesi 108 ,mitaji kwa washindi watano walioshindanishwa katika shindano la mapishi.