Na David John, TimesMajira Online, Dodoma
MGOMBEA Uspika wa Chama cha Alliance Democratic Change ADC Maimuna Said Kassimu amewaomba wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumpa kura za kutosha wakati wa uchaguzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni Bungeni Dodoma.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hii kutoka Dodoma ,Maimuna amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kwa kuwa ana uzoefu wa Uongozi tangu akiwa chuoni hadi kwenye Chama.
Amesema kilichomsukuma ni kutokana na uwezo alionao kupitia taaluma aliyonayo ambapo amesomea masuala ya siasa ngazi shahada, itakayomsaidia kuondoa mapungufu yaliyomo kwenye Bunge .
“Kupitia elimu yangu niliyonayo na uzoefu wa Uongozi kwenye Chama na hata nilipokuwa chuo kikuu Cha Dodoma itanisaidia niweze kuwaongoza wabunge kuhakikisha tunakuwa kitu kimoja na kuondoa matabaka ” amesema
Nakuongeza kuwa “Mwaka 2020 niligombea nafasi ya ubunge Jimbo la Kilindi ambapo nilipata kura Zaid ya 18000 ,na nimekuwa na Dhamira kubwa kuongoza Jamii hivyo endapo wakinipa nafasi hiyo nitahakikisha naliongezea hadhi na kuwafanya wabunge kuondoa tofauti zetu za kichama kwani wabunge wako kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi”amesema Maimuna.
Na kupitia Hali hiyo itasaidia wabunge Kutoa hoja zenye tija kwa wananchi na Taifa ,na kuwaongezea Imani Watanzania kuwa chombo hicho ni chao na kinaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo hasa kuishauri Serikali Katika masuala ya kimaendeleo na kuikosoa Serikali pale panapobidi.
Pia ameongeza kuwa kupitia nafasi hiyo ataenda kuhamasisha wananchi hususani wanawake kuchapa kazi ,kuwaweka pamoja ili waweze kujadili mambo ya maendeleo ili Taifa liweze kusonga mbele.
Naye Mkurugenzi wa Fedha Chama Cha ADC ,Hassan Mvungi akieleza mchakato ilivyokuwa mpaka kumsimamisha Mgombea huyo no baada ya Ofsi ya Bunge kuletewa barua ikiwataka kama wako tayari kwa zoezi hilo .
Kuwa mchakato huo ulifanyika ikiwa ni kutangaza nafasi hizo ambapo wagombea wawili walijitokeza kuchukua fomu ambaye ni Maimuna Said Kassimu pamoja na Gabriel Innocent ambapo Maimuna alikidhi vigezo vyote na kupitishwa kugombea nafasi hiyo.
Pia amesema kuwa tayari wamechukua vigezo vyote ambavyo vinawataka wagombea ambao sio wabunge kupitia Ofsi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na waliandaa barua na viambatanisho vyote na kuviwasilisha huku nao wakisubiri kukamilisha utaratibu wa Tume na kusubiri uchaguzi hiyo tarehe 1 February mwaka huu .
“Sisi kama ADC tumeona ni fursa kwetu ,tunamuamini Mgombea wetu ni mchapakazi ,mnyenyekevu, na muadilifu tuko pamoja nae na kupitia haya tunaimani atasimamia kanuni zilizopo kwani ana uwezo mkubwa “amesema Mvungi.
Hata hivyo alisema matarajio waliyonayo ni kuona Chama Cha ADC inakamata nafasi ya Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
More Stories
Tanzania,Uturuki kushirikiana kuinua sekta ya utalii nchini
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu