Na Bakari Lulela,TimesMajira Online, Dar
MGOMBEA wa kiti cha Udiwani kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), Kata ya Mbagala Dar es Salaam Juma Maanya amewaahidi wakazi wa eneo hilo kuwaboreshea miundombinu mara watakapomchagua kukitumikia kiti hicho katika uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika Julai 18, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kampeni ya kuomba kura kwa wananchi wa maeneo ya Jeshi la Wokovu amesema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza kata hiyo atahakikisha kuwa anaboresha miundombinu ya kata hiyo ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo.
“Ndugu zangu wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wakazi wa kata hii ninaomba ridhaa yenu ya kunichagua kwa kura za kutosha ili niweze kuwatumikia huku nikishirikiana na viongozi wenzangu katika kuwaletea maendeleo,” amesema Maanya.
Aidha Maanya amesema atakapopata nafasi ya kushika kiti hicho amejipanga kuwaletea fursa za kiuchumi wakazi hao sambamba na kuviinua vikundi mbalimbali vya wajasiriamali kwa kuwapa mikopo na kuhakikisha masuala ya ulinzi na usalama yanashika hatamu.
Hata hivyo mgombea huyo amewaomba wakazi wa Mbagala kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kwa lengo la kumchagua kwa kura nyingi ili aweze kuifanya Mbagala kuwa na maendeleo kama zilivyo kata zingine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam,Mama Kate Kamba amewasihi wakazi wa Mbagala wamchague Juma Maanya ili aweze kuwaletea maendeleo ndani ya kata hiyo ikiwemo kuwaboreshea miundombinu.
Kate Kamba amemnadi mgombea huyo kwa kusema ni msikivu,mwenye juhudi na mpenda maendeleo atayeweza kuwatumikia wakazi hao kwa kuwaletea maendeleo endelevu ndani ya kata hiyo.
More Stories
LALJI yatoa msaada wa sare na vifaa vya shule kwa yatima
Dkt.Biteko aagiza Kituo cha huduma kwa wateja Tanesco kusukwa upya
Rais Samia aridhishwa na uongozi safi wa Mwinyi