November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mfumo wa ‘Booking’ ya Matibabu kupunguza misongamano hospitalini

Na  Aveline Kitomary,TimesMajira Online,Dar es Salaam

Ni mara nyingi kumekuwa na tatizo la wagonjwa kufika hospitalini kwa kuchelewa  kutokana na sababu mbalimbali.

Mojawapo ya sababu ni uhaba wa fedha za matibabu ,wingi wa watu katika hospitali na pia ufahamu mdogo kuhusu dalili za magonjwa.

Lakini  kikubwa zaidi imekuwa ikilalamikiwa kuwa na msongamano wa wagonjwa hospitalini  hali inayosababisha kuwepo kwa foleni kubwa .

Hii inakuja baada ya hospitali kuzidiwa na idadi ya wagonjwa huku kukiwa hakuna ufahamu kuhusu hospitali zingine zinazoto huduma hizo.

Kwa sasa maisha yanabadili na teknolojia inaendelea kukua hasa katika nchi zilizoendelea ambapo kila huduma huwekwa ‘booking’.

Katika nchi hizo hata mgonjwa anapotakiwa kwenda kutibiwa kwanza lazima awe katika mfumo wa bima ya afya na pili kufanya booking kupitia mtandaoni kabla hajafika hospitali husika.

Kama abiria anavyoenda kukata tiketi mapema kabla ya kusafiri ndio huduma zingine zinavyoanza kutolewa hivyo hapa nchini.

Katika kulitatua tatizo la wagonjwa kushindwa kuchangua aina ya matibabu wanayotaka na hospitali teknolojia mpya nchini imeanzishwa ili kurahisisha mgonjwa kuweka booking.

Wakati wa Mahojiano maalum na Jarida la Afya ya Majira ,Mkurugenzi Mtendaji wa Afyayangu Company  Limited  Dkt Cyprian Ntomoka anasema kapuni hiyo imeazingua application mpya inayoitwa PASEDO app ikiwa na lengo la kuisaidia jamii kupata matibabu haraka.

“ PASEDO  ilizaliwa kwa sababu ya tatizo  mahali , mfano tatizo kwa wagomjwa ,Wagonjwa wengi wanakuja kwa hospitali wakiwa wnaumwa sana wengi wanaogopa kwenda hospitali kwa sababu si mahali  kirafiki zaidi kwao.

“Na sababu nyingine ni sehemu ambayo watu wengi hawafahamu na wengine wanakuwa na maswali mengi sana ikiwemo kuwaza kukuta foleni,madaktari wakoje. 

“Wagonjwa wanaumwa wanakwenda hosptali wanakwenda kwa kuchelewa kwa hiyo PASEDO inakuja kutatua tatizo hilo,”anasema Dkt Ntomoka.

Anaeleza kuwa mfumo huo wa booking kwa wagonjwa utasaidia vituo vya afya vilivyoshindwa kujiendesha na vingine kufungwa.

Mkurugenzi wa Afyayangu Company Limited Dkt Cyprian Ntomoka akionesha PASEDO App inavyofanya kazi

ITAWASAIDIA MADAKTARI

Dkt Ntomoka anasema kuna madaktari wanaenda sehemu za kazi lakini wanashindwa kuwaona wagonjwa kutokana na kutokujulikana kwa huduma zao.

Anasema pindi wakapojiunga na mfumo huo wanaweza kukutana na wagonjwa na kutumia taaluma zao kama inavyotakiwa.

“Kuna madaktari wanaend kwenye vituo vya kazi na kuchati , pia kuna madaktari ambao wanafanya kazi hospital za serikali ikifika saa tisa wanaondoka na kuacha wagonjwa wengi na kukimbilia vituo binafsi na kukuta hakuna wagonjwa na kukaa hivyo kupelekea ujuzi wa dakatari kupotea bure  kwa maana ujuzi kaacha kuutumia panapo husika .

“Lakini pia kuna madaktari wapya hawajulikani na wamekaa na ujuzi na kuna  namna wagonjwa wanatafuta madakari wanaowataka  na madaktari wanawatafuta wagonjwa na hawawapati.

“Mfano kuna wauguzi wengi wanaweza kusaidia kusafisha vidonda  ingefaa hata kufika nyumbani kwa mgonjwa kumsaidia  kusafisha vidonda ,Kuna watu wanapata stroke nyumbani ingefaa watu kwenda nyumbani kuwasaidia.

Anasema kuwepo kwa changamoto hizo katika sekta ya afya ni sababu ya kuanzishwa kwa kuhuduma hiyo.

“Hivyo PASEDO  ni matokeo ya tatizo , tunataka kutatua matatizo hayo kwa wahudumu wa afya na pia kwa wagonjwa.

INAVYOFANYA KAZI

Kwa Mujibu wa Dkt Ntomoka Application hiyo ina sehemu tatu ambayo ni ya mgonjwa, daktari na hospitali.

“Jambo la kwanza lazima mgonjwa na Daktari  wote  wanafikia mfumo wa pasedo kupitia simu zao za mkononi kwa sasa watatumia simu janja (smart phone ) unaenda kwenye playstore unapakua kama unavyopakua applicationi zingine kama whatsup au facebook.

“Baada ya hapo ukishaipata  kama ni mgonjwa  unajisajili baada ya hapo utaandika taarifa zako ikiwemo namba ya simu ,jinsi na kwende namba ya simu utapaswa kuanza na +255 na baada ya hapo application itakutumia password (nyiwila).

Anasema kwa upande wa dakatri anaweza kujiunga na mfumo huo kwa kujisajili kwa kuweka vyeti vyke na leseni ya kufanya kazi.

“Ila kama ni daktari  utapaswa kujisajili ila utatakiwa kuweka vyeti vyako kama Daktari ,leseni yako na ujuzi wako na elimu yake  ili kujilizisha juu ya taaluma yake.

“kwa  upande wa Hospitali lazima ijisajili kwa kupitia hiyo hiyo PASEDO application ila kwa pande wa hospitali lazima iingize  nakala ya usajili wa  wizara,”anaeleza Dkt Ntomoka.

ITAONDOA  MISONGAMANO  HOSPITALI

Dkt Ntomoka anasema faidia ya gteknolojia hiyo ni kumfanya mgonjwa aweze kuchagua akatibiwe hospitali gani.

“Kama anataka sehemu iliyo karibu pia anaweza akapata kwa mfano kama atatakaWilaya ya  Kinondoni akitafuta ataona hospitali zote za Wilaya ya Kinondoni zilizojisajili.

“Na anaweza kuchagua aina ya hospitali akitafuta hospitali ataona taarifa zote za hospitali kuanzia huduma wanazotoa na muda wa huduma kwahiyo atafanya booking hivyo ukituma wanakuwa na taarifa zako kuwa unaenda katika hospitali hiyo kupata huduma,”anafafanua.

Anasema kupitia mfumo huo kama mgonjwa hatajua hospitali anayohitaji iko wapi anaweza kuelekeza kwa ramani ya mtandaoni(google map).

“Kwa mfano kama unataka huduma meno unaweza kuenda pia kuchangua katika huduma zinazotolewa na hospitali na kama ni hospitali maalum kwa huduma unayotaka utasaidia.

“Kama utafanya booking wanaweza kukuambia muda wa kuenda hospitali hivyo hataenda kukaa foleni hospitali

 na kama utakuwa unahitaji dakatri bingwa labda tuseme bingwa wa ngozi ,meno,macho ukishatafuta hospitali zote zenye hizo huduma zilizojisajili zitaonekana.

“lakini pia kama unahitaji kutafuta daktari unayemtaka kama amejiunga na mfumo unampata na unaweza kujua anapatikana wapi na kwa muda gani hivyo unaweza kufanya booking,”anaeleza Dkt Ntomoka.

ITAWARAHISISHIA MADAKTARI

Dk Ntomoka anasema dakaktari ambaye amejisajili ataweza kumuona mgonjwa aliyefanya booking kupata huduma yake na kuweza kumjibu muda gani anaweza kupata huduma.

“Ukienda upande wa madaktari anajisajili na mfumo huo  na anaingia anakuta page yake atachagua hospitali anayohudumia wagonjwa wake lazima hospitaliiwe imesajiliwa katika mfumo itaonekana.

“kama kuna mgonjwa kafanya booking anaweza kumuona kupitia mfumo huu na ataona idadi ya wagonjwa na ataweza kugawa muda wake.

“kama siku hiyo hayupo amepata dharura anaweza kufunga page yake  na ikaonekana hayupo kazini,”anabainisha.

NI LAZIMA HOSPITALI KUJISAJILIA

Ili hospitali yoyote iweze kuonekana katika application hiyo Dkt Ntomoka anasema ni lazima iwe na ukarasa wake.

“Lazima na yenyewe ijisajili  kwa platform zao, mgonjwa akishafanya booking jina lake linaonekana katika hospitali na watajua leo tuna wagonjwa kiasi gani na kama wanaweza kuwahudumia.

“Na pia huduma zote zinazopatikana katika hospitali zitaonekana  ,kwasasa hakuna gharama za kujiunga ni bure,”anaeleza.

Anasema  lengo la application hiyo ni kutatua tatizo ambalo lipo katika jamii na kama itaonekana inajibu matakwa ya wananchi itawakuwa vizuri.

“Hii ni community application lazima ifikie jamii tunajitahidi kuwafikia kuaambia suluhisho la tatizo ambalo lipo baada ya kuona wagonjwa wanapata shida

hospitali wajiunge na mfumo na pia madaktari wajiunge na mfumo huo itakuwa rahisi kwao,”anasisitiza Dkt Ntomoka.