January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wafikia thamani ya Trilioni 5.2

Na Jackline Martin

Hali ya mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii ( NSSF) umeendelea kukua na kuongoza ambapo hadi sasa umefikia thamani ya Shilingi Trilioni 5.2

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mashomba wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa.

Mashomba alisema katika malipo ya mafao wamezidi kuwa juu na wanachama wanaostaafu wanafaidika;

“Katika ulipaji wa mafao tupo juu na wanachama wetu wanaostaafu wanafaidika na sisi kwasababu tunalipa mafao bila kuchelewa”

Aidha Mashomba alisema katika mfuko huo wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wanatoa huduma mbalimbali zinazopelekea wanachama kuridhishwa na huduma hizo;

“Huduma nyingine tunazotoa ikiwa ni pamoja na kujisajili zinakwenda vizuri hivyo wanachama wetu kwa ujumla wanaridhika na huduma zetu, na hasa katika kipindi hiki ambacho tunajikita hasa katika kutoa huduma za kimtandao wanafarijika sana kwasababu usumbufu mwingi unakua haupo”

Mbali na hayo mashomba alisema kuwa Kufuatia maadhimisho hayo ya huduma za fedha kitaifa NSSF wanatoa elimu mbalimbali ikiwemo elimu kuhusu hifadhi ya Jamii;

“Katika Banda letu tunatoa elimu kwa wanachama, elimu kuhusu hifadhi ya Jamii lakini pia umuhimu wa kujiwekea hifadhi hasa pale mtu anapokosa uwezo wa kufanya kazi kwa maana ya kuzeeka au pengine kupata majanga mfano ulemavu, Na huduma kuhusu huduma zetu tunazotoa kupitia mtandao”

Mshomba aliongeza kuwa shughuli zao zingine wanazozifanya katika kuwaelezea wanachi ni pamoja na masuala ya uwekezaji, lakini pia hata kwa wao jinsi ambavyo wanaweza kutumia mfuko wetu na kile ambacho wanaweza kuwapa baadae kwa maana ya mafao kuendelea kuwekeza zaidi”

Pia Mshomba alimazila kwa kusema elimu inayotolewa inawafikia na watu wa mikoani pia kwa kutumia huduma kupitia mtandao, vyombo mbalimbali vya habari kama Radio, TV na wakati mwingine maofisa wao kupitia ofisi zao za Mikoani wanawafikia kwa kuwatembelea katika sehemu zao za makazi.