Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mfanyabiashara ambaye ni Mkurugenzi Gravity Tax Consultance ,John Mwajulu pia Mwenyekiti wa Tabata Runners Club ,amechangia shilingi milioni 1tasilim shule ya Sekondari Kinyerezi, kwa ajili ya kuweka geti la shule hiyo kwa ajili ya usalama wa Mali za shule.
Mkurugenzi John Mwajulu, alitoa pesa hizo ,katika mahafali ya kidato cha nne wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu 231 wa shule ya sekondari ya Kinyerezi wilayani Ilala.
“Tunaisaidia Serikali kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan sera ya Elimu bure tunachangia shilingi millioni 1 tasilimu ili kutengeza geti la shule la sekondari ya Kinyerezi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa mazingira ya shule “alisema Mwajulu.
John Mwajulu alisema baki na kutoa msaada huo pia atafanya mazungumzo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jery Silaa awatafutie eneo la kujenga ukumbi wa mikutano wa kisasa ambao utakuwa unawaingizia kipato shule ya Kinyerezi uweze kutumika katika shughuli mbali mbali ikiwemo za kiserikali.
Mkurugenzi John Mwajulu pia alisema mikakati mingine kuboresha mazingira ya shule hiyo ikiwemo vyoo vya wanafunzi na Walimu kujenga vya kisasa na kutafuta wadau kuleta tanki la maji ya kunywa kwa ajili ya shule hiyo sambamba na kuboresha Ofisi ya Mkuu wa shule ikiwemo kuweka thamani za kisasa.
“Naunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya Elimu shule ziwe na mazingira bora ya kujifunzia na ufundishaji “alisema.
Akizungumza na wahitimu wa kidato cha nne katika shule hiyo aliwataka wakafanye vizuri katika masomo yao wachague masomo bora yatakayowavusha kusonga mbele waweze kupata ufaulu mzuri ambapo aliwaasa wawe na nidhamu na usikivu na kumtanguliza Mwenyezi Mungu.
Mkuu wa shule hiyo DANIEL MWAKYAMBIKI alisema shule ya sekondari Kinyerezi ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 96 wa kidato cha kwanza haya ni Mahafari ya kidato 14 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.
Mwalimu DANIEL MWAKYAMBIKI alisema shule hiyo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha nne idadi yao 1759 na wahitimu wa mwaka huu 2023 231 akizungumzia matokeo ya mtihani wa Taifa kwa miaka mitatu katika shule hiyo mwaka 2021 wanafunzi waliofaulu asilimia 67.5 mwaka 2022 waliofaulu asilimia 64 .5 na mwaka 2023 asilimia 86
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato