Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Thobias Makoba, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Makoba anachukua nafasi ya Mobhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine.
Kabla ya Uteuzi huu Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Kabla ya kujiunga na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Makoba alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Pamoja na kushiriki katika majukwaa mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo UN, African Union, SADC, EAC, World Economic Forum na mengineyo, kwa vipindi mbalimbali aliwahi kuwa Katibu wa Mawaziri wawili wa Mambo ya Nje Bernard Membe na baadae Balozi Dokta Augustine Mahiga kabla ya Kwenda kuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar.
Makoba ana Masters Degree in Security and Strategic Studies kutoka National Defence College – Tanzania, Post-Graduate Diploma in Economic Diplomacy kutoka Chuo Cha Diplomasia Kurasini na Degree ya kwanza ya Political Science and Sociology with majors in International Relations.
More Stories
Papa Francis afariki Jumatatu ya Pasaka akiwa na miaka 88
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni