December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto awapongeza wadau sekta ya Elimu

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji wamempongeza mdau sekta ya Elimu Kampuni ya Solar AG Energies com .ltd kwa kufunga umeme wa Solar shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko katika kutekeza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan .

Pongezi hizo cheti Cha Shukrani kilikabidhiwa na Meya Kumbilamoto Leo katika hafla Maalum ya kupongeza kampuni hiyo iliyofanyika shuleni ya Uhuru Mchanganyiko baada kufungiwa Solar katika vyumba vya kulala shule hiyo.

“Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inawapongeza wadau wetu katika sekta ya Elimu AG Energies com ltd kwa msaada wenu kufunga Solar katika shule hii ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya Wanafunzi wetu wa mahitaji Maalum ambao wanasoma shule hii awali walikuwa wakipata changamoto umeme unavyokatika Kila wakati.”alisema Kumbilamoto.

Kumbilamoto alisema Serikali inawatambua mchango wenu itashirikiana pamoja katika masuala ya Elimu katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kumbilamoto alisema Taifa lolote linategemea watu wake wapate Elimu Ili liweze kusonga mbele liwe na Maendeleo hivyo Halmashauri ya Jiji imeweka mikakati mizuri ya elimu kuanzia elimu ya awali ,Msingi mpaka Sekondari kwa Wananchi wake sambamba na ujenzi wa madarasa elimu ya Msingi na Sekondari.

Katika hatua nyingine Meya Kumbilamoto alisema ahadi nyingine ya MH,Rais shule ya BENJAMIN MKAPA imeshatekelezeka shule hiyo imeshaingiziwa milioni 200 akaunti ya shule kwa ajili ya ujenzi hivi karibuni Halmashauri itatangaza tenda .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Tabu Shaibu alipongeza wadau hao wa sekta ya Elimu Kwa juhudi zao kubwa kuwekeza sekta elimu Msingi .

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya AG Energies com ltd Ibrahim Musssen alisema wanaunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya Elimu katika kusaidia Jamii

Meneja Ibrahim alisema Kampuni yao Ina mifumo mbalimbali umeme wa Solar pamoja na taa walizofunga shuleni hapo warantee miaka miwili zinadumu kwa miaka minane.

Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko Sezaria Kiwango alisema shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ina wanafunzi 523 kati yao wavulana 369 wasichana 154 akizungumzia mafanikio kitaaluma Kila mwaka inafanya vizuri katika kufaurisha wanafunzi pamoja na kushinda tuzo mbalimbali za MAZINGIRA Bora ya shule yao.