Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amemtaka mkuu wa Idara ya Manunuzi Halmashauri ya jiji hilo kutatua changamoto zote za mfumo wa Manunuzi kwa njia ya Kielekroniki(NeST)
Meya Kumbilamoto alisema hayo kwenye ukumbi wa Mikutano Arnatoglou wilayani Ilala wakati wa kikao kilichohusisha watumishi kutoka Idara ya Elimu msingi,idara ya sekondari na sekta ya afya .
“Nakuagiza mkuu wa Idara ya Manunuzi tatua changamoto zote za mfumo wa manunuzi ya umma kwa njia ya kielecroniki ili miradi iliyopangwa kutekelezwa iweze kukamilika kwa wakati “alisema Kumbilamoto.
Meya Kumbilamoto alisema kikao hicho pia kimewasirikisha ugavi Manunuzi,Ujenzi, ambacho kililenga kujadili utekelezaji wa miradi ya Serikali ambayo imeelekezwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Meya Kumbilamoto alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyojitoa kuwahudumia wananchi na kutoa fedha za miradi ya maendeleo.
Aidha aliwataka Wakuu wa idara kusimamia miradi yote ya maendeleo iliyoelekezwa na Serikali ikiwemo miradi ya sekta ya Elimu, sekta ya afya ili iweze kuisha kwa wakati wananchi waweze kufurahia matunda ya Serikali yao.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi