Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa Genereta la kisasa kwa ajili ya mabucha ya nyama Vingunguti wilayani Ilala.
Meya Kumbilamoto amesema Genereta hiyo ina thamani ya shilingi milioni 50 itatumika katika mabucha hayo ya nyama yaliojengwa na Halmashauri ya Jiji hivi karibuni ambapo Sasa hivi yamekamilika .
“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mabucha yetu ya Vingunguti yaliojengwa kwa fedha za Serikali kutupatia Genereta ya shilingi milioni 50 ,Genereta hii itatumika wakati umeme umekatika ” alisema Kumbilamoto .
Meya Kumbilamoto aliwataka wafanyabiashara kutunza machinjio hayo vizuri na kufuata taratibu za Usafi Ili kuvutia wateja mbali mbali ambao watafika kununua nyama katika mabucha hayo ya kisasa .
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato