November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mdhibiti ubora ashangazwa na miundombinu St Anne Marie

Mkurugenzi wa shule za St Anne Marie Academy, Dk. Jasson Rweikiza akiwalisha keki wahitimu watarajiwa wa darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Elikana Manyilizu ambaye ni Mdhibiti Ubora wa Shule wa Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, akikabidhi cheti kwa mhitimu mtarajiwa wa darasa la saba shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam kwenye mahafali yao yaliyofanyika shuleni hapo siku ya Jumamosi
Elikana Manyilizu ambaye ni Mdhibiti Ubora wa Shule wa Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, akizungumza na wahitimu watarajiwa wa darasa la saba shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam kwenye mahafali yao yaliyofanyika shuleni hapo siku ya Jumamosi
Mkurugenzi wa shule ya St Anne Marie Academy iliyoko  Mbezi Kimara kwa Msuguri, Dk. Jasson Rweikiza, akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya darasal la saba ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo siku ya Jumamosi
Mwanamuziki maarufu nchini kama MADEE akilishwa keki kwenye mahafali ya darasa la saba ya shule ya St Anne Marie Academy

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM

SHULE ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam imepongezwa kwa kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya shule na kufanya vizuri kitaaluma mwaka hadi mwaka.

Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Elikana Manyilizu ambaye ni Mdhibiti Ubora wa Shule wa Manispaa ya Ubungo, wakati wa mahafali ya 20 ya shule ya msingi yaliyofanyika shuleni hapo.

Pia amewapongeza Maafisa wote wa Elimu wa wilaya ya Ubungo (Afisa Elimu kata- Msigani, Afisa Elimu Wilaya ya Ubungo na wasaidizi wao kwa kusimamia vizuri sana Elimu ndani ya Wilaya hiyo ya Ubungo.

Amesema usimamizi mzuri wa viongozi hawa unachangia sana shule hiyo ya St. Anne Marie Academy kuendelea kufanya vizuri kitaaluma.

“Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatambua mchango mkubwa wa shule ya St. Anne Marie Academy pamoja na shule nyingine za binafsi, tutaendelea kuweka mazingira rafiki ili kupata shule nyingi ziweze kuwekeza kwenye elimu na kutoa huduma zilizotukuka kama za St. Anne Marie Academy,” amrsema.

Amesema ana imani kuwa mafanikio hayo makubwa ya shule yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wafanyakazi wa shule hiyo, kujituma, kufanya kazi kwa bidii na uwekezaji mkubwa uliofanywa na uongozi wa shule, Naomba msirudi nyuma endeleeni kufanya kazi zenu kwa bidii ili shule hii iendelee kupaa siku hadi siku.

Amewapongeza wanafunzi wanaohitimu kwa kufanikiwa kuifikia siku hiyo na kwamba walikuwa na nidhamu nzuri, mlikuwa mnasoma kwa bidii, mlifanya vizuri sana katika mitihani mbalimbali. Kwa mwenendo huu ni matumaini yangu kuwa mtafanya vizuri sana katika mitihani ya Taifa Mnayotarajia kufanya hivi karibuni.

“Napenda kupongeza sana uongozi wa shule kwa usimamizi mzuri wa shule. Sote ni mashahidi kwamba shule hii inafanya vizuri sana kitaaluma kwa kupata matokeo mazuri sana katika mitihani ya Taifa. Nimesikia hapa kwenye taarifa kwamba matokeo ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita ni mazuri sana,” amesema.

Amesema matokeo haya makubwa yanaonesha ni kwa jinsi gani shule hii imejipanga kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanaohitimu hapa wanapata matokeo mazuri sana na kwamba hilo ni jambo kubwa sana na serikali inatoa pongezi kubwa.

Wakati huo huo, shule ya Msingi na Sekondari, St. Anne Marie Academy kwa mara nyingine imesisitiza kwamba hakuna mwanafunzi hata mmoja atakayerudishwa nyumbani kwa kushindwa kulipa ada baada ya kufiwa na mzazi.

Msimamo huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza, kwenye mahafali yha 20 ya shule ya msingi yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

“Kwa mwaka 2021 pekee wazazi 40 walifariki lakini watoto wao wote wanaendelea na shule hakuna hata mmoja ambaye amefukuzwa. Tumeona tufanye hivi kwasababu baada ya mzazi au mlezi kufariki watoto wanahaingaika sana,” alisema Dk. Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijinini (CCM).

“Mpango huu ulianza mwaka 2019 na mwaka 2020 wakati wa korona wazazi 42 walikufa ilikuwa ni kilio kikubwa sana kwetu na kwa watoto tukaona tubuni mpango mwanafunzi akishaingia hapa St Anne Marie akafiwa na mzazi wake au mlipa ada ataendelea kusoma hapa hatafukuzwa,” amesema

Dk. Rweikiza amesema jambo lingine wanalojivunia ni kuwalea wanafunzi hao kwenye maadili ya hali ya juu na kwamba hali hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa katika kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya kiwilaya, mkoa na yale ya kitaifa.

Amesema kuna viongozi wa dini zote ambao wamekuwa wakitoa mafundisho ya dini na wanafunzi wote wanalazimika kuhudhiria ibada za imani zao kila zinapokuwa kwenye shule hiyo.

“Hapa tunafundisha kama hatuna akili nzuri kwasababu kazi yetu ni kufaulisha tu kila mwaka tunahakikisha wanafunzi wanafaulu kwa viwango vya hali ya juu hatutaki wazazi walipe ada wasifurajie matokeo mazuri,” amesema

Pia Dk. Rweikiza amesema wataendelea kuibua vipaji vya wanafunzi ili wawe watu maarufu kwa kufanyakazi za sanaa kama muziki wa kuimba, mitindo na fasheni.