December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mchango sekta ya uvuvi kufikia asilimia tatu ifikapo 2030

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

MCHANGO wa sekta ya uvuvi kwenye uchumi wa nchi kwa sasa umefikia asilimi 1.9 ambapo lengo la wizara ni ifikapo mwaka 2030 uwe
unachangia zaidi ya asilimia tatu lengo
likiwa ni kufika asilimia 10

Mchango huo utakwenda kukua kutokana na mabadiliko makubwa ya kisera na ya kisheria yanayotarajiwa kufanyika na vile vile uboreshwaji wa miundombinu sambamba na
kuwawezesha wavuvi.

Hayo yalisema jana na waziri wa Mifugo na Uvuvi , Abdallah Ulega wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano nane wa Mawaziri wa Uvuvi, Bahari na Maji ya ndani kwa
nchi wanachama wa umoja wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) ulioanza jana na kutarajiwa kumalizika septba 13 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

“Kila mmoja anafahamu jitihada za Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya utoaji boti za Kisasa ambazo ni za mkopo nafuu na kila mmoja anafahamu juu ya ujenzi wa bandari ya uvuvi kwani uvuvi wa bahari kuu tumeshindwa
kukamata ile fursa kwa muda mrefu ni kwasababu ya kukosena na bandari nzuri ya uvuvi tunashukuru maono ya rais samia kwani yamekuwa ni moja kwa moja ya ujenzi wa bandari ile na tayari tumefikia asilimia 60 ya uje zi wake”

Kutokana na hivyo, Waziri Ulega alisema meli kubwa za kimataifa zitakuja kutia nanga kwasababu hapo awali hazikuwa na mahali sahihi pa kutia nanga.

Pia alisema wanatarajia kuwa kuwa na viwanda vya uchakataji ambavyo vitakwenda kuiinua sekta hiyo hasa katika kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.

“Kwamba wakishaleta yale mazao basi yachakatwe hapa hivyo itapelekea kupatikana kwa ajira kwa vijana wa kitanzania na tutakua tumeongeza thamani , tutakusanya kodi na ushuru mbalimbali, lengo ni kuwaona wavuvi
wenyewe waweze kuboresha hali zao”

Kuhusu, Mwendeno wa uuzaji nje wa mazao ya uvuvi waziri ulega alisema wamekuwa wakienda vizuri ambapo kwa mwaka 2019-2023 wanatakribani trilioni 2.2 ikiwa ni thamani ya samaki waliowauza ambapo ushuru wa serikali ni takribani bilioni 98.4 Pia kwa mwaka 2023-24 takribani tani 42,245.16 zenye thamani ya bilioni 193.9 huku ushuru wa serikali ikiwa ni bilioni 13.7

Kwa upande wake Afisa Kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juma Nzima alisema wako katika mkutano huo lengo ikiwa ni kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji namna ya kuzipata lakini pia kuziendea


“Tunatangaza fursa kwenye upande wa uvuvi zaidi na uchumi wa buluu, ikiwemo utengenezaji wa boti za uvuvi, uzalishaji wa mazao mbalimbali ya baharini na kwenye maziwa kama ufugaji samaki, pia utengenezaji wa vifaa vya kuvulia samaki, utengenezaji wa
vifaa au maeneo ya kuhifadhia samaki au mazao yanayoendana na uvuvi kwa ujumla wake” Alisema

Mkutano huo unalengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuwawezesha wavuvi wadogo ukizingatia mabadiliko ya tabia nchi naukuaji wa idadi ya watu inayoendelea,
kubadilishana uzoevu na mataifa mengine duniani lakini pia kutangaza utalii wa ndani.