Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema usafiri wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam yanatarajia kuanza hivi karibuni kubeba abiria mara baada barabara ya Mwendo kasi kukamilika ambapo yatasafirisha abiria masaa 24 usiku na mchana katika jimbo la Ilala.
Mbunge Mussa Zungu, alisema hayo wakati wa Uzinduzi wa umoja wa wanawake wafanyabiashara wa soko la Ilala Sokoni UWAWASOI jimboni Ilala, uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji ambapo awali wanawake hao walikuwa wakilalamika kupoteza muda mrefu katika changamoto ya huduma za usafiri.
“Nawapongeza wanawake wa mama Lishe wa Ilala kwa kumchangia fomu ya Urais Shilingi milioni moja Dkt.Samia Suluhu Hassan, mwanamke mwenezu akachukullie fomu ya Urais kwani ni kazi kubwa mmefanya kutokana na kupato chenu kuwa kidogo kutokana na pesa hiyo hiyo Mgambo wa Halmashauri ya jiji nao kuchukua “alisema Mbunge Zungu.
Mbunge Zungu aliwataka wanawake wa Jimbo la Ilala wampe kura za Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya,sekta ya Elimu na kuboresha miundombinu ya Barabara ambapo kwa sasa Barabara zote zinawekwa lami.
Katika hatua nyingine Mbunge Zungu amewataka Maafisa maendeleo wa kata na Maafisa Maendeleo wa Wilaya kugawa fedha kwa vikundi vya Wanawake wa Ilala mara mikopo hiyo ya Serikali itakapotoka rasmi.
Aliwataka Madiwani wa Jimbo la Ilala na Wenyeviti wake wa Serikali ya Mtaa kushirikiana pamoja na kusimamia wanawake na vikundi viweze kuwezeshwa mikopo hiyo ya asilimia kumi ambayo inatokewa ngazi ya Halmashauri
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â