January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Zungu atoa majiko 200 ya gesi kwa mama Lishe Ilala

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu amegawa majiko 200 ya gesi kwa mama Lishe wa masoko jimboni Ilala Ili watumie nishati mbadala waache kutumia kuni katika kupika chakula .

Akigawa majiko ya gesi leo kwa mama Lishe wa soko la Machinga Complex Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, amesema Rais wa Dkt .Samia Suluhu Hassan anajali afya za Wafanyabiashara wa mama lishe kwa kuwagawia majiko Ili kurahisisha mapishi waache kutumia mapishi ya kutumia Moshi ni hatari katika afya .

“Tumegawa majiko ya gesi kwa mama lishe wa Ilala ,soko la Machinga Complex ,Ilala Boma ,Mchikichini na gerezani mama lishe itawasaidia kupika chakula na kupasha moto kila wakati kwa wateja wao itawavutia Biashara zao ” amesema Zungu .

Mbunge Zungu amewataka waondokane na kasumba kwamba chakula ukipika na gesi sio kizuri badala yake watumie gesi katika mapishi yao mapishi ya gesi hayana Moshi na chakula kinakuwa kisafi .

Amesema mapishi ya mama lishe wakitumia gesi inaokoa pesa kwa kutumia nishati mbadala pia hawawezi kupata ugonjwa wa kifua kikuu .

Alisema hewa ya ukaa inaenda angani kuharibu Mazingira majiko ya gesi watu watakuwa salama bila kupata magonjwa na Mazingira hayawezi kuharibika .

Meneja wa Soko la Machinga Complex Stella Mgumia, amepongeza Serikali na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, kugawa majiko ya gesi kwa mama Lishe wa Machinga Complex .

Meneja Stella Mgumia amewataka wafanya Biashara wanaofanya Biashara maeneo si rasmi kuondoka maeneo hayo kwenda kufanya biashara zao Machinga Complex na wauza chips na mihogo waliopo pembeni mwa Barabara ya Kawawa kuondoka maeneo hayo .

Aliwataka wafanyabiadhara kufanya biashara zao katika soko la Machinga complex kuna fursa mbalimbali za kukuza Uchumi .