December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Zungu amezitaka Halmashauri kuangalia suala la matibabu ya Wazee

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, amezitaka Halmashauri Nchini kuangalia suala matibabu ya Wazee waweze kupata huduma Bora za matibabu .

Naibu Spika Zungu aliyasema hayo akiwa Jimbo la Ilala kuzindua Baraza la Wazee Kata Kisutu .

Alisema huduma za matibabu ya Wazee katika vituo vya afya ni KERO amna kituo cha afya ambacho kinawapa kipaumbele wazee katika suala zima la matibabu nchini.

“Naomba Halmashauri kutazama upya suala la matibabu ya Wazee waweze kupata huduma Bora za afya wafikapo hospitali nashangazwa vituo vya afya wanashindwa kutambua Wazee wakati Hospitali zote Mali ya Serikali “alisema Zungu.

Ameagiza utolewe waraka wa Serikali wa kutambua Wazee katika matibabu bila kupewa KERO wawapo kituo cha afya .

Mbunge Zungu alisema Sera ya Taifa Mabaraza ya Wazee yapo kisheria kila kata kwa ajili ya kusaidia serikali na inatambua umuhimu wao.

Mbunge Zungu alisema Wazee wanatakiwa kuunda mabaraza yao alafu kutoa ushauri katika kusaidia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Katika hatua nyingine Mbunge Zungu alisema kuna vijana wanagombana na Wazazi wao wanashindwa kuwa nao karibu wakati watoto wao wamesoma .

Aliagiza wazee washirikishwe katika miradi ya Serikali katika Utekelezaji wa Ilani na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mwaka jana alikutana na wazee wote kuzungumza nao na mwaka huu pia atakutana nao ni sehemu ya utaratibu wake kuzungumza na wazee.

Akizungumzia Bima ya Afya iliyoboreshwa Mbunge Zungu alisema imewatambua wazee pamoja na makundi maalum wakiwemo walemavu.

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu akizungumza na wazee wa Kata ya Kisutu Wilayani Ilala wakati wa kuzindua baraza la kata (kushoto)Mwenyekiti wa CCM Wilaya Said Sidde na Diwani wa Kisutu Khery Kessy .Picha na Heri Shaaban.
Wazee wa Kata ya kisutu wakimsikiliza Mbunge wa Ilala Mussa Zungu