Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MBUNGE wa Embakasi Mashariki Nchini Kenya,Dkt Paul Owino maarufu Babu Owino amewataka vijanawa kitanzania kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika changuzi zijazo ikiwa ni pamoja kuwa waandilifu ili waweze kuaminika kushika nyadhifa hizo.
Dkt Owino ametoa wito huo jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la Ngome ya Vijana lililokwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti, Katibu, pamoja nafasi nyengine mbalimbali.
Dkt Owino amesema mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo ni fursa nzuri wa vijana wa kitanzania kuchangamkia ikiwa ni pamoja na kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo za ubunge.
“Vijana mnapaswa kutambua kuwa nyinyi ni viongozi wa Leo na si kesho hivyo tumieni uchaguzi ujao kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali “amesema
Nakuongeza kuwa
“Chama cha ACT Wazalendo ni cha kuigwa kutokana na kuwa chama bora chenye mfumo imara wa kupigania haki na kuwalea vijana ambao wana uwezo wa kukipigania kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla”
Awali katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amewataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi ambao wataweza kuwaongoza wananchi, kukitetea na kukijenga Chama hicho .
“Chama hiki kinawategemea sana vijana kwani wamekua wakiwalea kwenye misingi iliyoimara ya uongozi na kimewaamini ndio maana hawategemei wanachama ambao wanatoka kwenye vyama vyengine kwenda kujinga kwao bali wanachagua viongozi waliowalea wenyewe”amesema Shaibu
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi