Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi ameitaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini ( TARURA ) kuhakikisha inafanya kila jitihada ya kutatua changamoto za Barabara korofi kwa kuzikarabati ili kuwawezesha wananchi waweze kufanyaka kazi zao za kuitafuta riziki bila matatizo yoyote.
Mbunge Janeth ametoa agizo hilo katika ziara yake
katika Jimbo la Ukonga kwa kukagua miradi ya maendeleo , kuzungumza na wananchi kwenye maeneo yao wanayoishi pamoja na kutoa misaada ya majiko ya gesi kwa wanawake Wajasiriamali jimboni humo.
Mbunge Masaburi akiwa Mtaa wa Bangulo Kata ya Pugu Station, amejionea ubovu wa barabara za ndani zilivyoharibika kutokana na mvua zinavyoendelea kunyesha na hivyo kuleta kadhia kwa wananchi kushindwa kupitia kwenye barabara hizo kwa ajili ya kufanya shughuli zao za maendeleo.
“Barabara hizi zimekuwa na changamoto kwa hiyo ndugu zangu wa TARURA na Taasisi zingine zinazohusika na barabara natoa agizo marekebisho ili wananchi waweze kuhishi kwa amani”amesema Masaburi
Mbunge Janeth Masaburi amewataka wananchi wa jimbo la Ukonga kuwa na subira Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatekeleza Ilani kwa vitendo hivyo aungwe mkono .
Wakati huo huo amegawa majiko kwa Mama Lishe wa Kigogo Fresh na Bangulo Wajasiriamali na aliwataka
Wasitumie nishati ya Mkaa badala yake watumie nishati mbadala na gesi wasiharibu mazingira waunge mkono juhudi za Rais katika utunzaji mazingira.
Naye Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Reginal Mashanda amesema wanatambua kuwepo kwa changamoto za Barabara kwenye mitaa mbalimbali ikiwemo Kata ya Bangulo, hivyo kuhusu hiyo barabara imeshafanyiwa usanifu na hivyo ipo kwenye mpango wa kutengezwa.
“TARURA ina mpango wa muda mrefu na muda mfupi wa ujengaji wa barabara hizo, sema mvua zinazoendelea kunyesha ndiyo zinatukwamisha mipango yetu kutokwenda sawa, lakini kwa hivi sasa tutaweza kuzitatua changamoto hizo kwa kuleta gari ya kunyonya maji na kisha kuweka kifusi kwenye barabara hizo”amesema Mhandisi Martin.
Akizungumza kuhusiana na changamoto wanayoipata kwenye barabara za kwenye mitaa yake, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bangulo Kata ya Pugu Station Goolick Mweri ameiomba (TARURA) ifanye jitihada ya kuwasaidia wananchi wa Kata hiyo ili waweze kuendelea kuwa na Imani na Serikali yao.
Nao baadhi ya wananchi akiwemo mwana bodaboda Stambuli Juma amesema barabara zao ni mbovu hivyo ameiomba Serikali iweze kutatua changamoto hiyo kwani imekuwa vigumu kwao kwani wanapowabeba aburia wamekuwa wakiwaangusha kutokana na ubovu wa barabara.
Janeth Masaburi amefanya ziara kutembelea wananchi wanaopatwa na changamoto ya Barabara eneo la Ulongoni B, Bonde la mpunga, kwa Muhogo mchungu, zahanati ya Bangulo, Kituo cha Afya cha Pugu Kajiungeni na Soko la Biashara la Pugu, Jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa