January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Masaburi agawa majiko ya gesi kwa mama lishe

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es salaam Janeth Masaburi, amegawa majiko ya gesi kwa mama lishe na Baba Lishe katika masoko mbali mbali mkoa Dar es Salaam kwa ajili ya kuhamasisha watumie nishati ya gesi na mkaa mbadala.

Akizungumza katika soko la Mbagala Rangi tatu kwa wabisora Mbunge Masaburi, alisema Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan inawataka watanzania watumie gesi na nishati mbadala waache kutumia mkaa na ukataji misitu ni wanaharibifu wa mazingira katika nchi yetu .

“Tunamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kuamasisha matumizi ya gesi na nishati mbadala nawaomba mama Lishe na Baba Lishe mtumie Nishati ya gesi na mkaa mbadala muwache kutumia mkaa na ukataji miti ovyo nchi yetu itakuwa janga ni uharibifu wa mazingira “alisema Masaburi.

Mbunge Masaburi alisema dhumuni la ziara hiyo katika mkoa Dar es Salaam kuangalia miradi ya maendeleo ya Serikali na masoko kuangalia changamoto za wafanyabishara na kuzungumza ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wake.

Aliwataka Mama Lishe na Baba Lishe wajenge tabia ya kuweka fedha katika vibubu ili waweze kununua majiko ya kisasa ya gesi kwa matumizi yao mbalimbali.

Aidha alisema matumizi ya gesi ni salama kwa afya unapotumia uwezi kupata hewa chafu unapotumia matumizi yake ni salama kiafya.

Aliwataka mama lishe wa Mbagala Rangi tatu soko la Wabisora kujenga tabia ya kuwa wasafi katika biashara zao ili wateja wawavutie kila wakati, na kuwataka maafisa Biashara Temeke kuwachukulia hatua wachafuzi wa mazingira wapigwe faini wawe wasafi.

Meneja wa masoko wilaya ya Temeke ambaye ni Msimamizi mkuu wa masoko ya Manispaa hiyo Godfrey Asukile alisema soko la Mbagala Rangi tatu lina wafanyabishara 750 ambapo anaipongeza Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan wameboresha soko hilo kwa Milioni 500 ambapo kwa sasa limeboreshwa lina mpangilio mzuri .

Meneja Godfrey alisema kwa sasa Serikali inajenga soko la Tandika,Temeke Stereo na keko mikakati yake imeanza katika masoko hayo makubwa yatakuwa ya kisasa .