Na Mwandishi Wetu, Timesmajira OnlineĀ
MBUNGE Neema Lugangira ameongoza Maandamano ya Wanawake wa Kagera Kupinga Ukatili Dhidi ya Albino na kufika Msibani Kata ya Kamachumu, Wilaya ya Muleba, Kagera.
Aidha, Mhe Neema Lugangira amewasilisha Salaam za Pole kutoka kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuwahikishia Wananchi kuwa Serikali kupitia Jeshi la Polisi ipo kazini kuhakikisha waliohusika wote watapatikana na haki inatendeka.
Aidha, Mbunge Lugangira ameahidi waombolezaji kutafuta wadau na kuanzisha Kampeni ya Kuelimisha Jamii kuhusu kulinda wenzetu wenye ualbino, kukataa kutumika na kupinga vikali ukatili wa aina zote kwa albino.
Mhe Neema Lugangira aliambatana na Katibu wa UWT Mkoa Kagera, Mwenyekiti UWT Wilaya ya Muleba, Katibu UWT Wilaya ya Muleba, Madiwani Viti Maalum kutoka Wilaya ya Muleba na Wanachama wa UWT na CCM.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Mtoto Asimwe Mahala Pema Peponi, Amina.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato