November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Kishimba aipongeza Serikali kutoa Mahindi ya chakula Kwa Bei nafuu Kwa wananchi wake

Na David John, TimesMajira Online

MBUNGE wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba amesema kuwa wameaza kupokea mahindi Kwa ajili ya chakula na tayari Tani 100 za mahindi zimeshapokelewa na wataendelea kupokea Tani zingine zipatazo 1000.ambazo zitasaidia wananchi Kwa kipindi hiki ambacho bado Kuna changamoto ya chakula.

Amesema kuwa wanamshukuri Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuleta Mahindi hayo Kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kupata chakula kitakachowasaidia wananchi Kwa kipindi hiki ambacho wanatarajia kwenda kuvuna mazao miezi ijayo.

Kishimba ameyasema hayo wilayani kahama wakati akishuhudia wananchi wakinunua Mahindi Kwa Bei elekezi ya Serikali ya shilingi 15000 Kwa debe Moja lenye ujazo wa kilo 20. Ambapo amesema kuwa Bei hiyo inaweza kusaidia kupunguza mfumuko wa Bei mitaani hususani kwenye maeneo ya Luzewe,katoro mkoani Geita pamoja na Kagongwa wilayani humo ambalo wanalima Mahindi Kwa wingi.

“Tunaomba wananchi wa maeneo mengine ambako wataaza kupeleka Mahindi Siku chache zijazo wawe wavumilivu lakini pia kama wataweza kuja hapa kahama Mjini nawaje “amesema Kishimba

Mbunge huyo amekiri.kwamba Hali ya chakula Kwa wananchi wa Jimbo ilikuwa mbaya sana kwasababu debe Moja la Mahindi lilikuwa linauzwa Kwa Bei ya shilingi 25000 ambayo ni Bei ya juu kabisa kuwahi kuishuhudia ambapo Mahindi ya Serikali yanauzwa Kwa Bei ya shilingi 15000 Kwa debe sawa na nusu ya Bei ya awali.

Amesema kuwa baada ya Serikali kuleta ahueni ya Bei ya Mahindi Kwa wananchi hivi mitaani Bei imeaza kupungua na hiyo ni baada ya wafanyabiashara kugundua kuwa Serikali imeaza kuleta Mahindi Kwa wananchi wake.

“Kutokana na Hali hii tunatarajia inaweza kitusaidia kabla hatujapata chakula kingine Kwa maana ya kuvuna hivyo tunaendelea kuwahimiza wananchi wajikite zaidi kwenye uzalishaji hasa wakati huu ambapo inaonekana kama mvua zinaendelea kunyesha na kwasababu wananchi wajimbo hili ni wachapa kazi.”amesema Kishimba

Ameongeza kuwa wananchi hao ni wazalishaji wazuri wa mazao ya Mahindi ,karanga ,mpunga na mazao mbalimbali na wakati wowote ndani ya wiki zijazo baadhi ya mazao yataaza kuvunwa kwahiyo tatizo la njaa litapungua kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo akizungumza ruhusa mikutano Kwa vyama upinzani amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuviomba vyama vyote nchini kutumia fursa hiyo kuelezea mazuri yanayofanywa na Serikali lakini pia kueleza sera zao mbele ya wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu kupokea Mahindi ya chakula kutoka Serikalini Kwa ajili ya wananchi wilayani humo ili kupunguza ukali chakula.