November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Kembaki-Watoto acheni kuingilia ugomvi wa wazazi wenu

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Wito umetolewa kwa watoto ambao wazazi na walezi wao wanagomban a mara kwa mara kuacha tabia ya kuingilia ugomvi kwani wanapoingilia inawafanya kuathirika zaidi kifikra lakini pia kuwashushia wazazi heshima

tabia hiyo ya ugomvi mara nyingi huzaaa maadili mabaya lakini pia huchangia mmonyoko wa maadili kwa kiwango kikubwa sana

hayo yameelezwa na mbunge wa jimbo la Tarime mjini Bw Maiko Kembaki,ambaye pia ni mkurugenzi wa shule za Ghati Memorial pamoja na Nyahiri,wakati akiongea na wanafunzi,walezi,pamoja na wazazi kwenye maafali ya darasa la saba pamoja na Sekondari ya shule ya awali pamoja na msingi ya Nyahiri iliopo Jijini Arusha

Kembaki alisema kuwa kwa sasa ndani ya jamii nyingi kumekuwa na tabia ya mama na baba wakigombana basi watoto wanaingilia au wananunua ugomvi huo jambo ambalo sio sawa

Alisema kuwa hali hiyo inachangia kwa kiwango kikubwa sana kushusha kiwango cha nidhamu kutoja kwa watoto kuja kwa wazazi.

“ugomvi unapotokea mara nyingi watoto watasimama kwa mzazi ambaye ana nguvu hata kama amekosea na watoto sasa watapambana kweli kuhakikisha wanamchukia au kumdharau sasa nawaambia kuwa mnakosea kazi yenu ni kuwaheshimu wazazi na sio kuwadharau”alisema Kembaki.

Pia aliwasihu wazazi kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kuwaaambia watoto wao wanawapenda kwani wakati mwingine neno nakupenda limekuwa kama kigezo cha kuwafanya watoto kuangukia kwenye mikono mibaya.

“tujifunze kuwaaambia watoto tena hasa mabinti kuwa mnawapenda neno la nakupenda ni muhimu sana kwa watoto au vijana wetu”aliongeza Kembaki

Naye Jackson Nikumwitika akiongea kwenye maafali hayo kwa niaba ya mkuu wa shule ya msingi na Sekondari alisema kuwa jukumu la malezi na maadili mema sio la walimu pekee bali hata wazazi nao wanatakiwa kulisimamia ipasavyo

Nikumwitika aliwaasa wazazi kuhakikisha kuwa wanakuwa na tabia njema ambazo watoto wataziiga na kuachana na tabia zenye maadili mabaya

Alihitimisha kwa kusema kuwa watanzania sasa wanatakiwa kuwapeleka watoto kwenye shule ya nyahiri msingi pamoja na sekondari kwa kuwa wana mikakati mizuri ya kuwapa elimu yenye kiwango cha juu lakini pia kuwafundisha maadili ambayo yanafaaa