January 18, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Jerry Silaa awaasa wanamichezo Jimbo la Segerea

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Segerea

Mbunge wa Jimbo la Ukonga ,Jerry Silaa ,amewaasa wana michezo wa Jimbo la Segerea timu zilizoshiriki michezo ya kugombea kombe la Bonah Cup 2022.

Mbunge Jerry aliwaasa vijana hao wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Tabata shule ambapo timu ya Madereva wa Bajaj walipambana na Bodadoda .

“Michezo ujenga afya,michezo ni ajira nawaomba wananchi wa Segerea tutumie michezo hiii vizuri tuweze kukisemea vizuri chama chetu cha mapinduzi na kumsemea vizuri Mbunge wetu wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, ambaye ametoa ajira katika sekta hii ya Michezo ” alisema Jery Silaa.

Mbunge Jerry alisema Mbunge Bonah Kamoli anajituma Sana katika kuleta maendeleo jimboni ikiwemo kuwaunganisha Wananchi pamoja katika sekta ya michezo .

Aidha aliwataka Wananchi wa Segerea pia kuunga mkono kazi za Utekelezaji wa Ilani zinazofanywa na Mh,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mbunge wa Segerea Bonah Kamoli alisema ufunguzi wa michezo hiyo inashirikisha timu zote za Kata 13 za Jimbo la Segerea pamoja na Mitaa yake.

Mashindano hayo ya Bonah Cup, yanashirikisha mpira miguu na Rede kwa wanawake wa Jimbo la Segerea yatafanyika katika Viwanja tofauti .