November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonnah ataka Mikopo ya Halmashauri Wananchi wakope Jimbo la Segerea

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, amesema mikopo ya Serikali ya asilimia kumi inayotolewa ngazi ya Halmashauri ameomba irudi haraka Ili Wananchi wa Jimbo la Segerea waweze kukopa wajikwamue kiuchumiMbunge Bonnah Kamoli alisema hayo Buguguni katika mkutano wa hadhara wakati wa kuzungumza na Wananchi wa Jimbo hilo.

“Mikopo ya asilimia kumi imekuwa kero Wananchi wanalalamika tunaomba iweze kurudi Wananchi wa Jimbo langu waweze kukopa wajishughulishe katika kukuza mitaji ya Biashara wajikwamue Uchumi ” alisema Bonnah.

Mbunge Bonnah pia alielezea kero maji ya safi ya DAWASA Kata ya Buguruni ameomba DAWASA kutatua changamoto hiyo Wananchi waweze kupata maji safi na salama malalamiko yapungue ya kudai maji ya DAWASA .

Wakati huo huo aliitaka Serikali kuharakisha malipo ya fidia ya Kipunguni Kata ya Kipawa kupisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Wananchi walipwe wapishe eneo hilo ambalo waliliacha zaidi ya miaka 25 bila kuendelezwa baada Serikali kuzuia kuendeleza ujenzi kupisha upanuzi wa uwanja huo toka mwaka 1997.

Akielezea mikakati yake katika Jimbo la Segerea alisema kila Kata wanatarajia kujenga vituo vya afya vya Serikali kwa ajili ya kutoa huduma za Afya ,ambapo baadhi ya Kata vituo vya afya vinajengwa na vingine ujenzi upo katika hatua za mwisho .

Akizungumzia sekta ya Elimu katika Jimbo la Segerea alisema kila Kata kuna shule ya Serikali imejengwa.

Katika hatua nyingine alisema mradi wa kuboresha Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP)tayari umesainiwa ametaka uwanze ujenzi huo uanze haraka kutengeza Barabara za Jimbo hilo kwa ajili ya kutatua kero .

Kwa upande wake Diwani wa Kata Minazi Mirefu GODLSTEN MALISA aliomba serikali iwapatie eneo la Hali ya hewa kwa ajili ya kujenga shule ya Kata hiyo .

Diwani wa Kata Mnyamani SHUKURU DEGE alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Segerea kuwajengea shule ya Msingi Mnyamani katika kata hiyo ameweka historia miaka yote aina shule ya Msingi wala Sekondari .

Diwani Shukuru Dege aliomba Serikali iwajengee barabara za ndani ikiwemo Barabara ya Plan kuelekea Hospitali ya Serikali .

Wananchi wanapata shida wakati wa kupeleka wagonjwa Hospitali Barabara hiyo Miundombinu yake sio rafiki .

Diwani BUSORO PAZI alielezea baadhi ya mafanikio ya Kata ya Buguruni yaliofanywa na Mbunge BONNAH KAMOLI wamepokea shilingi Bilioni 5.5 za maendeleo kwa ajili ya miundombinu mfereji wa maji mkubwa ,soko la Buguruni limekarabatiwa kwa shilingi bilioni 1. wamepokea Madawati 500 ya shule kutoka Halmashauri ,pesa za makusanyo ya ndani vikundi Kumi vilipata mkopo .

Aidha Diwani Busoro alisema walipokea shilingi milioni 300 za elimu Miradi yote hiyo ni Utekelezaji wa Juhudi za Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na sasa mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi Barabara inajengwa ya Mwendo Kasi magari ya Daladala yataanzia Buguruni kwenda Posta .Mwisho