January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonnah ashauri kata ya Kinyerezi igawanywe

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli,ameshauri kata ya Kinyerezi iliyopo Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam igawanywe kata ya pili iitwe KIFURU kutokana ukubwa wa eneo hilo wananchi waweze kupata huduma za jamii karibu na makazi yao.

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli, alitoa ushauri huo katika ziara yake ya Jimbo la segerea kuangalia miundombinu ya Barabara, shule,na miradi ya Serikali iliyopo jimboni humo.

“Nashauri Mtaa wa KIFURU kata ya Kinyerezi igawanywe iwe kata mpya kutokana ukubwa wa kata hiyo iwe kata ambayo inajitegemea wananchi wa KIFURU waweze kupata huduma za jamii karibu na makazi yao wasisumbuke kwenda mbali ,nawaomba viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kinyerezi muwanze Mchakato wa kuomba kugawanywa haraka “alisema Bonah.

Mbunge Bonnah alisema kata KIFURU ikiwagawanywa wananchi watabaki KIFURU kwa ajili ya kupata huduma za Serikali na za kijamii awawezi kwenda Kinyerezi ni mbali na makazi yao.

Katika ziara hiyo Mbunge Bonnah na wataalam wa TARURA, na viongozi wa Halmashauri walitembelea Barabara ya Kichangani, Daraja la Majoka kata ya Kinyerezi, Daraja la majoka,Barabara ya Kichangani, Majengo ya Baba Lishe,na Mama lishe Vingunguti na Barabara ya Faru kata ya Mnyamani

Katika hatua nyingine Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli, alisema Daraja la Majoka Kinyerezi limejengwa kwa fedha za Halmashauri bado alijakamilika kwa sasa ,Barabara hiyo itakuwa ya kisasa itafungwa Taa ameshukuru uongozi wa Halmashauri na Meya wa jiji kwa kuwezesha fedha za ujenzi huo.

Diwani wa Kata ya Kinyerezi Leah Mgitu amesema Mtaa wa Kichangani kero yao kubwa Miundombinu ya Barabara inayoelekea Zimbili ikijengwa Barabara hiyo kero itaisha ,changamoto nyingine ameshauri fidia ifanyike kwa ajili ya huduma za Jamii,ikiwemo Zahanati,Shule ya msingi.

Diwani Leah mgitu aliwataka wananchi wa Kinyerezi Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kutoa ushirikiano mara mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji utakapoanza DMDP ili Kinyerezi yao iwe ya kisasa.

Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto alisema Halmashauri hiyo wamepokea zaidi ya billion 200 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa sasa ,Halmashauri hiyo ina Mkurugenzi makini Jomary Mrisho Satura wanakusanya mapato vizuri kero zote zitatatuliwa Kinyerezi.

Meya Kumbilamoto alimpongeza Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo na kusimamia miradi ya Serikali iliyopo jimboni humo.