Na Herishaban, TimesMajira Online
Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli amepokea vifaa tiba vya shilingi millioni 300,000,000 katika jimbo la segerea kwa ajili ya vituo vya afya vitatu .
Mbunge Bonnah alipokea vifaa hivyo Dar es Salaam jana katika vituo vya afya Segerea, Kinyerezi na Kiwalani ambapo kila kituo cha afya vifaa vya shilingi milioni 100,,000,000
Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli alipongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya afya na kujali afya za wananchi.
“Awali wananchi wangu wa jimbo la segerea walikuwa wanaenda Mnyamani katika hospitali ya Plani kwa sasa huduma za upasuaji zinapatikana katika vituo vyote vitatu Segerea, Kinyerezi na Kiwalani pamoja na huduma za mama na Mtoto “alisema.
Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli alimpongeza mganga mfawidhi wa Kiwalani amesimamia vizuri mradi huo mpaka umemalizika pamoja na changamoto ya Maji mradi umeisha kwa wakati.
Mbunge Bonnah alimpongeza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji hilo kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Serikali yote ambapo amesimamia vizuri utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapunduzi CCM ili kwa ajili ya kuwaeleza wananchi utekelezaji wa Ilani.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Dkt. Zaituni Hamza, alisema vifaa tiba vyote thamani yake shilingi millioni 300,000 000 kila kituo cha afya vifaa vya shilingi milioni 100,,000,000 ambapo kila kituo wamepokea shuka 200 Kinyerezi na Kiwalani na kituo cha afya Segerea shuka 500 .
Dkt, Zaituni Hamza alisema kituo cha afya Kinyerezi wamepokea vitanda,mashuka,will cheir na Segerea wamepokea Vitanda ,magodoro, shuka will cheir kazi zote wanazofanya ni utekelezaji wa Ilani katika kutekeleza Ilani ya chama cha Mapunduzi CCM.
Dkt, Zaituni alisema vituo hivyo vya afya vinatarajia kuzinduliwa hivi karibuni baada taratibu za kupata vifaa tiba kukamilika .
Diwani wa viti Maalum Moza Mwano alipongeza Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya afya na sekta ya Elimu nchini ambapo alisema wanajivunia katika nchi yetu kazi nzuri ya kuendelea kusimamia wananchi.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua