Na Moses Ng’wat,TimesmajiraOnline,Songwe.
MBUNGE wa jimbo la Songwe mkoani Songwe, Philipo Mulugo,ameiomba serikali kujenga daraja katika Mto Kikamba ambao ana historia nao kutokana na wazazi wake wote wawili Baba na Mama kufariki kwa kuliwa na mamba wakati wakivuka katika mto huo.
Mulugo aliwasilisha ombi hilo, Mei 27, 2024 kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kukaguzi ujenzi wa nyumba ya walimu (Two in One) katika shule ya sekondari ya Philipo Mulugo iliyopo katika kijiji cha Udinde, kata ya Udinde na kuzungumza na Wananchi ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu Wilayani inayolenga kukagua miradi ya maendeleo, pamoja na kuzungumza na wananchi.
Ombi kama hilo la kutaka kujengwe daraja katika mto huo pia lilitolewa juzi na Askofu Jimbo Kuu la Mbeya ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu nchink(TEC) Askofu Gervas Nyaisango kwa Waziri Mkuu.Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ibada maalum ya kuwekwa wakfu Askofu msaidizi Godfrey Mwasekaga.
Akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kusalimia mbunge huyo alitumia fursa hiyo kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chongolo kusaidia kutia msukumo wa upatikaji wa fedha kwa ajili ya kujengwa daraja katika mto huo ili kunusuru wananchi kupoteza maisha kwa kuliwa na Mamba.
“Kupitia wewe Mkuu wa Mkoa kwa sababu wewe ndiye Rais wa Mkoa wa Songwe unaemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan tunaomba sana tupate daraja katika mto kikamba kati ya Rukwa na Udinde”,alisema
“Mimi kama mbunge nimeomba sana kwani toka mwaka 2010 nilipoingia ubunge nimekuwa nikisema na hatimaye katika kusema siku moja Mama yangu mzazi aliyenizaa mimi kwa kukamatwa na mamba na isitoshe miaka kumi tena baba yangu mzazi naye alikufa baada ya kukamatwa na mamba katika mto huo” alieleza kwa uchungu Mbunge Mulugo.
Mama mzazi wa mbunge huyo, Christina Kadiago, ndiye alianza kufariki kwa kuliwa na mamba mwaka 1991 na baadaye mwaka 2006 alifariki Baba yake kwa kuliwa na mamba katika mto huo.
Baada ya ombi hilo la mbunge, Mkuu wa Mkoa alimtaka Meneja wa Wakala wa barabara mijini na Vijijini (Tarura) Mkoa wa Songwe, Mhandisi Kilian Haule kueleza mipango ya Tarura katika kutatua changamoto hiyo.
Mhandisi Haule alisema kuwa, mpango wa dharura wa Tarura ni kujenga kivuko cha kuning’inia maarufu kama kiteputepu ambapo tayari shilingi milioni 300 zimeombwa.
Akizungumzia ujenzi wa daraja la kudumu katika mto huo, Mhandisi Haule alisema mchakato wa kuanza kazi ya usanifu wa daraja hilo unatarajia kuanza mapema julai mwaka huu kwa ajili ya kupata gharama halisi za ujenzi wa daraja hilo.
“Mkuu wa Mkoa ukiacha ujenzi wa kivuko cha dharura (kiteputepu) tayari wataalam kutoka makao makuu tukawapeleka pale na wakaona na nikaagizwa niandike barua ya kuomba fedha kwa ajili ya kazi za usanifu na tukikamilisha tutajua gharama halisi na tutaleta kwako ili utusaudie kutafuta fedha” alisema Mhandisi Haule.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Chongolo alisema kazi ya serikali ni kuwalinda wananchi na kuahidi kuchukua hatua za dharura ili kupatikana kwa kivuko cha muda kabla ya msimu wa mvua ujao.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi