Na Thomas Kiani, Timesmajiraonline, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mgharibi, Elibariki Kingu, amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuwapeleka madaktari bigwa watano kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wananchi katika Kituo cha Afya cha Sepuka.
Madaktari bingwa hao wametoa huduma za afya kwa wananchi katika Kituo cha Afya cha Sepuka kupitia kampeni ya Madaktari Bingwa wa Samia, inayolenga kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi.
Hatua hiyo inasaidia kuwaondolea usumbufu wananchi wa kusafiri kwenye hosptali za rufaa kufuata huduma hizo na wengi walizikosa kutokana na kutokuwa na uwezo.
Mbunge Kingu amemshukuru Rais Samia kwa kupeleka madaktari bingwa kwenye jimbo lake, ambapo wagonjwa 346 walipata huduma mbalimbali.
Amesema Serikali imeipa hadhi kubwa Wilaya ya Ikungi na Kituo cha Afya Sepuka, kwani ujio wa madaktari bigwa hao umewezesha kituo kuwa na vifaa tiba vya kutosha, dawa na vifaa tiba vya kutosha.
Mganga Mfawidhi, Dkt. Kessia Daniel amesema kituo chake kimepokea neema na heshima kubwa kutokana na ujio wa madaktari hao, kwani kituo hicho kimeweza kupatiwa dawa za kutosha pamoja na vifaa tiba.
Amesema kituo hicho kwa sasa kinahudumia wagojwa wa idara ya nje 400 hadi 500 kwa mwezi, kinalaza wagojwa 120 kwa mwezi, akinahudumia akina mama 80 wanaojifungua kwa mwezi.
Kwa upande wa kliniki amesema kituo kinapokea akina mama wajawazito na watoto 500 kwa mwezi wakiwemo wanaohudumiwa kliniki tembezi.
Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi, Lawrence Kijazi amesema ujio wa madaktari hao umeleta neema kubwa Ikungi na Kituo cha Afya Sepuka.
Kijazi ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuwapeleka madaktari hao na kukipa hadhi na wananch wamebufaika kwa ujio wao kwani sasa kuna vifaa tiba vya kutosha.
Akizungumza na madaktari hao, Kingu amewataka wafike tena mara nyingine kwa sababu huduma zao bado zinahitajika sana kwa watu wengi.
Baadhi ya wananchi wa Sepuka, wamesema matatizo yao yaliisha muda mfupi sana baada ya kukutana na madakitari hao, hivyo aliwataka warudi tena.
More Stories
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta