Na Moses Ng’wat,Timesmajiraonline,Mbozi.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbozi kupitia mapato yake ya ndani imegawa taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa wanafunzi 34827 wa shule za sekondari na msingi Wilayani humo.
Zoezi hilo la ugawaji wa taulo hizo za kike limefanyika Septemba 19, 2023 , chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe, ambapo amesema upatikanaji wa taulo za kike kwa wanafunzi ni msaada mkubwa kwao katika kufanya vizuri kitaaluma kwa sababu hawatakosa vipindi vya masomo bali watahudhuria vyote.
“Naomba niwasisitize walimu wenzangu na wanafunzi katika Wilaya ya Mbozi tuhakikishe tunatokomeza divisheni ziro na four kwani inawezekana sana na penye nia pana njia,”amesisitiza Mkuu wa Wilaya Mahawe.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema lengo la Halmashauri hiyo kutoa taulo za kike zinalenga kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi wa kike na kuongeza Ari na kujiamini katika kipindi chote cha masomo na maandalizi ya mitihani yao .
“Kusema ukweli kazi inafanyika katika awamu ya sita chini ya kiongozi wetu Mama Samia Suluhu Hassan…sasa hivi mnasoma katika mazingira rafiki sana madarasa yana tiles ya vioo vyoo vizuri huwezi kulinganisha kabisa na sisi tulikotoka,
“Sasa ninyi leo sijui mtakuwa na excuse gani mnasoma katika mazingira mazuri.
Lakini zamani mwanafunzi wakike katika siku zile 194 anazotakiwa kuwepo shuleni karibu siku 50 alikuwa anashindwa kufika shuleni akiingia katika ule mzunguko anashindwa kuja shuleni kwasababu mazingira hayajakaa vizuri,”ameeleza Mahawe.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba