December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbilinyi akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Pakistan nchini Tanzania

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kaimu Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Salvator Marcus Mbilinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Siraj Ahmed Khan jijini Dar Es Salaam Juni 24, 2024.

Wakati wa mazungumzo hayo viongozi hao walisaini Muhtasari wa Makubaliano ya Mashauriano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Pakistan (Agreed Minutes of the Bilateral Political Consultations-BPC).

Makubaliano hayo ambayo majadiliano yake yalifanyika mwezi Machi 2024 yaligusia ushirikiano kwenye biashara; uwekezaji; elimu; sayansi, teknolojia; mafunzo ya kujengeana uwezo; ulinzi, usalama; utamaduni na masuala ya kikonseli.

Kwa ujumla Makubaliano hayo yalilenga kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kwa faida na mustakabali bora wa nchi hizi mbili.