November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbarali kushirikiana na madiwani kumaliza kero ya ukosefu wa madawati

Na Esther Macha,Timesmajira,Online ,Mbarali

UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya umesema kuwa utashirikiana na madiwani wa Halmashauri hiyo katika kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi atakayekaa chini wilayani humo kutokana na ukosefu wa madawati.

Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Twalibu Lubandamo akizungumza na watumishi wa kata ya Imalilo Songwe

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ambaye pia ni Diwani wa kata ya Itamboleo,Twalibu Lubandamo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kikata ilifanyika katika Kata ya Imalilo Songwe.

Lubandamo amesema kuwa alipoingia madarakani kama Mwenyekiti wa halmashauri kipaumbele chake kikubwa kilikuwa madawati .

“Kwanini nasema hivi kwa sababu nilitembelea shule kadhaa za sekondari wilayani hapa na kushuhudia wanafunzi wanakaa chini,,mwanafunzi anahitaji kukaa kwenye dawati ili aweze kupata elimu ,hivyo kufika mwezi wa sita mwaka suala la wanafunzi kukaa chini litakuwa limekwisha”amesema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake,Diwani wa kata ya Imalilo Songwe ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Chuki Mbwanjine amewaomba wafanyakazi wanaopata changamoto katika maeneo yao ya kazi kutoa taarifa ili kuona jinsi ya kuwasaidia,pia kwa mvivu yeyote akibainika hawatasita kumchukulia hatua stahiki kwa kushirikiana na mamlaka husika ngazi za wilaya.

Hata hivyo Mbwanjine aliwaomba wenyeviti na watendaji wa vijiji kuwa pamoja kwa kujitahidi kujenga makazie ya wafanyakazi hasa walimu angalau nyumba moja kwa mwaka kwenye vijiji vyao ili walimu waweze kukaa maeneo ya kazie na kutekeleza majukumu yaoe kwa ufanisi na kwamba asimilia kubwa ya wafanyakazi waliopo kwenye kata zaoe wanakaa mbali na makazie yao ya kazi.

Diwani viti Maalum kata ya Mawindi,Catherine Atilio aliwataka wafanyakazi kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopesheka.

Diwani huyo amefafanua kuwa ili kumwondoa mfanyakazi katika ugumu wa maisha upo muhimu wa kuona namna ya kuunda vikundi baina yao ili kuwapa nafasi ya mikopo ya ujasiliamali mdogo.