January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mawaziri wakutana kuimarisha mikakati ya Kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ahimiza ushirikishwaji wa wadau wote katika kuunganisha nguvu ili kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiongoza kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa kisekta kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, kilicholenga kuimarisha mikakati ya kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.

“Waziri Simbachawene, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na wataalamu waandae miongozo yote izungumze kwa pamoja kuhusu ukatili wa kijinsia na baada ya kikao cha Mawaziri ushauri upelekwe kwa Waziri Mkuu ili aridhie.”

Ili hatua za muda mfupi hatua za muda wa kati na hatua za muda mrefu ziweze kuchukuliwa katika kupambana na vita hii, binadamu wamekuwa waajabu kuliko wanyama matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yanafanywa na ndugu wa karibu.

Katika kikao hicho amesema Mwaka 2021 viliripotiwa vitendo vya unyanyasaji wa watoto 110499 ni asilimia chache yawalioripoti.

“Uliongoza ni ukatili wa ubakaji 5899 na waliolawitiwa 1114 na waliopata mimba za utotoni ni 1677 na utafiti ukaonesha namba hizi uzigawe kwa 60, utaona asilimia 60 inafanyika nyumbani walipo baba na mama ndugu jamaa na marafiki na asilimia 40 ni nje ya nyumbani, wakiwa shuleni au wanapoenda shuleni.”

Lazima tuimarishe mifumo izungumze na uwajibikaji, sheria tunazo tayari tuna miongozo mbalimbali sasa tunahitaji mawasiliano yaanzie kwa Mawaziri yashuke kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, ishuke kwenye kata zetu, ishuke kwenye mitaa na vijiji.

“Mfumo wa mawasiliano uende kwenye kamati za mabaraza ya madiwani kwenye Halmashauri zetu, lakini kwenye vikao vya maendeleo vya kata ili viwe na nguvu ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ili hata marekebisho ya sheria ndogo ndogo yaanzie kule chini,” alisema Waziri Gwajima.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiongoza kikao cha Mawaziri wa Kisekta kilicholenga kuimarisha mikakati ya kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Doroth Gwajima (kulia) katika kikao
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa Adolf Mkenda (Kushoto) katika kikao