Na Martha Fatael, TimesMajira Online, Hai
NAIBU waziri wa Kilimo Anthony Mavunde,amesema serikali imekusudia kuboresha vituo vya utafiti sanjari na kuwawezesha watafiti kufanya kazi kwa ufanisi kama njia kuu ya kuboresha sekta ya kilimo nchini.Kadhalika serikali imetaka taasisi ya utafiti wa zao la Kahawa (TaCRI) iliyopo Lyamungo wilayani Hai, kujipanga ili kufikia lengo la uzalishaji wa miche Mil 20 kwa ajili ya kusambazwa kwa wakulima nchini.
Mavunde amesema hayo mwisho mwa wiki alipofanya ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya TaCRI kujua changamoto na mafanikio yake ili serikali iiongezee nguvu zaidi.
“Katika nyakati zote sasa wizara ya Kilimo tunakwenda na utekelezaji wa mipango madhubuti tunayojiwekea, tunasema Kilimo ni Uti wa mgongo wa Taifa,tunataka Hilo lionekane kwa vitendo” anasema.
Amesema serikali inakusudia kuwawezesha watafiti ili waongeze ufanisi na matokeo yao yabadili sekta ya kilimo nchini kama ilivyo azma ya Rais Samia Suluhu Hassan.Naibu waziri alitaka TaCRI kuhakikisha teknolojia pamoja na elimu vinawafikia wakulima nchini kwa wakati, ili waendesha kilimo chenye Tija.
Kwa upande wake,mkurugenzi wa TaCRI, Dkt Deusdedit Kilambo amesema katika suala la uzalishaji kwa kipindi cha mwaka 2022/23 wamelenga kuzalisha Miche 20,293,720 katika vituo vyake sita katika mikoa tofauti nchini.Dkt Kilambo ametaja vituo hivyo na kiwango cha Miche kitakachozalishwa kuwa ni Lyamungo (3,475,300), Ugano (3,348,429), Mbimba (5,110,000), Maruku (5,000,000), Mwayaya (1,715,000) na Sirari (1,645,000).
Amesema maeneo hayo yamegawanyika katika ukubwa tofauti wa utafiti wa Kahawa ambapo Lyamungo Ina ukubwa Hekta 148.13 na eneo la Kahawa ni Hekta 64.13.Mbimba hekta 156.0 yenye Kahawa ni hekta 18, Ugano Hekta 12 zenye Kahawa Hekta 4, Mwayaya Hekta 78.5 yenye Kahawa ni hekta 4.8 na Sirari Hekta 4.04 yenye Kahawa ni Hekta 2.04.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda