September 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maudhui ya kielektroniki mafunzo ya walimu yaandaliwa

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ipo katika mchakato wa kuandaa Moduli Saba zenye maudhui ya kielektroniki ili ziweze kutumiwa na walimu wa Elimu ya Msingi na Sekondari katika mpango wa MEWAKA katika mfumo wa ujifunzaji ujulikanao kama “Learning Management System” (LMS).

Kazi hiyo inafanyika kuanzia tarehe 12/12/2022 na kutarajiwa kumalizika tarehe 24/12/2022 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Morogoro.

Akifungua kikaokazi hicho, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Habari na Machapisho TET Bwana. Kwangu Masalu amesema kuwa, lengo la kuandaa maudhui hayo katika mfumo wa kielektroniki ni kurahisisha upatikanaji wa moduli hizo kwa walimu na kuwezesha ujifunzaji binafsi wa walimu wakiwa katika vituo vyao vya kazi kupitia simu janja au vishikwambi.

Aidha, Bwana Kwangu ameeleza kuwa kazi hiyo inafanywa kwa ushiriki wa Maofisa kutoka TET, CoICT (College of Information and Computer Technology) Walimu, Wakufunzi na Wataalamu kutoka mashirika binafsi

“Kazi hii inafanywa kwa ushirikiano na wataalamu mbalimbali hivyo ninawasisitiza washiriki wote wa kazi hii mfanye kazi kwa ushirikiano, kujituma na weledi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa” amesema Bwana Kwangu.

Vilevile Bwana Kwangu aliongeza kuwa kila mmoja wa washiriki anapaswa kujua kuwa ameaminiwa ili kuifanya kazi hii na hivyo inampasa kutunza dhamana hiyo kubwa kwa kujituma na kuzingatia usiri wa kazi.

Kwa upande wake mratibu wa kazi hiyo Bwana Japhet Magumbo amesema TET inaandaa moduli aina 7 ambazo ni; Elimu Maalum Moduli ya Elimu ya Stadi za Maisha, Moduli ya Ufundishaji na Ujifunzaji, na moduli ya Upimaji, Tathmini na utoaji wa Mrejesho.Elimu ya Msingi Darasa la V-VII Moduli za ufundishaji na Ujifunzaji, Stadi za Maisha na Moduli ya upimaji,tathmini na utoaji wa mrejesho pamoja na,English language module for upper primary school teachers.

Awali TET iliandaa moduli 10 za Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) chini ya mradi wa kukuza stadi za Kusoma, Kuandika, na Kuhesabu (KKK) ambazo zinalenga kukuza umahiri wa walimu katika kutekeleza mtaala wa Elimu msingi. Na Moduli 7 miongini mwa hizo hizo ndizo zinaandaliwa maudhui