November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashirika yanayojishughulisha na wenye ulemavu yatakiwa kujitokeza

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetoa wito kwa mashirika yote nchini yanayoshughulika na masuala ya wenye ulemavu kujitokeza ili kujulikana huduma wanazozitoa na kwa kiasi gani ili serikali iweze kushirikiana nao katika kutoa huduma hizo.

Hayo yasemwa jijini hapa leo Novemba 28,2023 na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za utengamao,tiba shufwaa na afya ya wazee,kutoka Wizara ya Afya Makao Makuu, Dkt.Mwinyi Kondo Amiri wakati akifungua kikao cha Mtandao wa utoaji huduma za utengamao ngazi ya Jamii (CBR Network) kilichowakutanisha wadau mbalimbali kutoka Serikalini na taasisi mbalimbali wakiwemo,Wizara ya Afya,Ofisi ya Waziri Mkuu,Tamisemi,Wizara ya Elimu na Wizara ya maendeleo ya jamii.

Wingine ni wadau wanaoshughulika na huduma za Elimu kwa watoto wenye ulemavu , huduma za utengamao,kusaidia watoto wenye mahitaji maalum nchini.

“Nitoe wito kwa mashirika yote nchini kujitokeza kuungana na mashirika mengine ambayo tayari yameshajitokeza yapo katika mtandao wa CRB ili kuweza kushirikiana kutoa huduma katika kundi hili la walemavu kwani mashirika yanatofautiana jinsi ya kufanyakazi hivyo wanapokuwa pamoja wanasaidiana ujunzi ambao mwingine anao na mwingine hana na kufikia malengo yanayatarajiwa na Serikali,”amesema.

Dkt.Amiri amesema kuwa CBR Network wanatoa huduma ni moja ya vipaumbele 14 vya Wizara ya afya vilivyosomwa kwenye bajeti ya wizara iliyowasilishwa rasmi na Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu katika bajeti ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24 hivyo vyema kushirikiana kwa pamoja ili tujue hata wasiojulikana kupata takwimu za watu wanaowahudumia ili kuweza kusaidia kama serikali katika mpango wake kwa watu wenye ulemavu.

Aidha ameeleza maana ya huduma za utengamao ambayo anashughulikia na CRB wanashughulikia kuwa ni huduma ambazo wanapata watu wenye matatizo tofauti ikiwemo wahanga wa masuala ya walemavu na ulemavu unaweza ukawa ulemavu wa kuzaliwa au ulemavu wa kurithi au ulemavu utokanao na shughuli za kibinadamu ambao utokana na ajali watu kupoteza viungo na wakuzaliwa nao ni ule kama watoto wenye vichwa vikubwa,wanaozaliwa na mgongo wazi au wanaozaliwa na aina ya ulemavu wa aina tofauti.

“Tunapozungumzia huduma za utengamao zipo zile ambazo zinatolewa kwa kufuata mfumo rasmi wa serikali kwa maana ya kutolea huduma za afya vya serikali lakini pia kuna mitandao ya watoa huduma hizi ambao ni mashirika au taasisi za kujitegemea yani NGOs,

“NGOs hizi zimejiunga na kutengeza mtandao wao ambao zinajiita CBR Network lengo likiwa ni kutoa huduma hizi za Utengamao kwenye ngazi ya msingi nchi nzima na lengo la kutoa huduma hizi kwamba wao wanalenga kuwafikia wananchi pale walipo ambao wanamahitaji hayo na sikwajili ya kuhudumia tu bali waanangalia pia masuala ya kiuchumi kwa kuwajengea uwezo kiuchumi ,kisaikolojia lakini pia kuwapatia vifaa wezeshi ili kuweza kutoa huduma zao za msingi,”ameeleza.

Ametaja vifaa wezeshi hivyo kuwa ni vile vya huduma za usikivu,uoni,vilevile masuala ya ujongezu kwahiyo mtandao huo unatoa huduma hizo kulingana na uwezo waliokuwa nao pia na dhima ya shirika pale lilipo kwani kuna ambao wanatoa huduma za usikivu tu,kuna wanaotoa huduma za uoni lakini kuna wanaotoa huduma za ujongevu.

“Vilevile kuna wanatoa huduma hizi kwa ujumla wake na kushirikiana na taasisi za kiserikali kwahiyo tunatambua mchango wao kama serikali kwasababu lengo la serikali ni kumuhudumia mwananchi na haya mashirika yana umoja wao unaolenga kutoa huduma hizi kwa wananchi ndiyo maana tupo nao pamoja na tunatambua mchango wao kwa serikali ,”amesema Dkt.Amiri

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtandao huo Elirehema Kaaya,alitaja lengo la kukutana kwenye kikao hicho cha mwaka 2023 na mkutano mkuu wa mtandao wa CRB wenye Mashirika takribani 24
ni kuleta nguvu ya pamoja kuungana na serikali kuona nanmna ambayo wanaweza kutoa huduma kwa pamoja na kwa ubora kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali.

“Kikao chetu ni cha siku mbili ikiwa ni mkutano mkuu lakini ni kikao kazi kujadili namna gani tunaweza kuendelea mbele kwa mwaka ujao na kwa miaka mingine ambayo inakuja mbele ili kuona namna gani tunaweza kuboresha huduma za utengamao katika ngazi za msingi.