January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashindano ya NBAA yazidi kushika kasi yatinga hatua ya Nusu fainali

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

MASHINDANO ya mpira wa miguu ya maadhimisho ya miaka 50 NBAA yaendelea kupamba moto baada ya hatua ya mtoano kukamilika kwa timu nne pekee kutinga nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea katika viwanja vya TPDC jijini Dar es salaam.

Nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kutimua vumbi siku ya Jumapili ya Novemba 20 mwaka huu ambapo itawakutanisha PWC dhidi ya KPMG majira ya saa 10 jioni katika viwanja vya TPDC jijini Dar es salaam

Kivumbi kingine cha kukata na shoka cha nusu fainali ya pili kitakuwa siku ya Jumatatu ya Novemba 21, majira ya saa 10 jioni kwa kuwakutanisha PKF na Techno Auditors katika viwanja vya TPDC jijini Dar es salaam.

Hivyo, ikumbukwe michuano hiyo ni kuelekea kilele cha miaka 50 ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania NBAA ambayo wameandaa mashindano hayo kama shamrashamra katika kuadhimisha miaka hiyo.